Monday, August 19, 2013

BBA Updates: Bimp na Angelo waiaga The Chase, Nigeria yafanikiwa kuingia Top 5 na washiriki wake wote wawili

Baada ya Bimp na Angelo kutolewa jana (August 18) hatimaye sasa The Chase imefikia hatua ambayo mtu unaweza kucheza karata zako na kubashiri mshindi, japo bado sio rahisi sana sababu chochote kinaweza kutokea ndani ya siku 6 zilizosalia.
Angelo n Bimp
Angelo na Bimp
Bimp ndio alikuwa wa kwanza kujua hatima yake kwenye Big Brother siku ya jana, baada ya IK kumtaja na huo ndio ukawa mwisho wa safari yake akiwa mshiriki wa 21 kutoka, na baadaye jina la Angelo lilifuatia na kukamilisha idadi ya washiriki wawili waliopaswa kuondoka usiku huo.
Katika kura za wiki iliyoisha Dillish ambaye pia alikuwa kikaangoni aliongoza kwa kura za nchi 7, akifuatiwa na Angelo na Bimp ambao wote walipata kura 4 kila mmoja ambazo hazikutosha kumuokoa yeyote kati yao.
Nchi ambazo zimeweka historia katika Big Brother ‘The Chase’ mwaka huu mpaka sasa ni Nigeria na Ghana. Nigeria imeweka historia kwanza kwa washiriki wake wote wawili Beverly na Melvin kufanikiwa kufika Top 5 na kuingia fainali, na pili Beverly amefanikiwa kuucheza mchezo kwa siku 86 (leo), na mpaka siku ya fainali zitakuwa 91 bila kuwa nominated wala kuingia dangerzone.
Elikem ambaye ndiye mshiriki wa kwanza kuingia Top 5 katika The Chase ameweka historia kwa kuwa mshiriki wa kwanza kuifikisha Ghana katika fainali toka mashindano ya Big Brother Afrika yaanze.
Washiriki wengine walioingia Top 5 ni mnamibia Dillish, Elikem wa Ghana na Cleo wa Zambia.
Unaweza kuanza kubashiri kwa Top 5 hii unahisi nani ana nafasi ya kuondoka na $300,000 za msimu wa nane wa Big Brother Africa ‘The Chase’ Jumapili hii?
Hivi ndivyo Afrika ilivyopiga kura
Angola: Bimp
Botswana: Angelo
Ghana: Dillish
Kenya: Dillish
Ethiopia: Bimp
Malawi: Bimp
Namibia: Dillish
Nigeria: Dillish
South Africa: Angelo
Sierra Leone: Dillish
Tanzania: Bimp
Uganda: Dillish
Zambia: Angelo
Zimbabwe: Dillish
Rest of Africa: Angelo
Total: Dillish = 7, Angelo = 4, Bimp = 4.
(Total: 15 Votes)

No comments:

Post a Comment

ShareThis