Katie Gee na Kirstie Trup, wakiwa na umri wa miaka 18 raia wa uingereza waliokuwa wakifanya kazi ya kujitolea kama walimu huko kisiwani zanzibar
Wasichana hao wawili walimwagiwa tindikali katika maeneo ya Mji Mkongwe wakiwa katika matembezi ya kawaida juzi usiku.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,
Mkadamu Khamis Mkadamu alisema tukio hilo lilifanywa na vijana wawili
waliokuwa wakiendesha pikipiki aina ya Vespa.
Mkadamu alisema Wazungu hao walikuwa walimu wa kujitolea katika Shule St Monica, Tomondo, Zanzibar.
Alisema waathirika hao wamedhurika kiasi kikubwa
katika maeneo ya kifua na mikononi na baada ya tukio hilo, walipelekwa
Hospitali Kuu ya Zanzibar na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Aga Khan,
Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Mganga Mkuu wa Aga Khan, Dk Jaffery Dharsee
alikataa kuzungumza chochote kuhusiana na hali za wasichana hao akisema
hajapata ruhusa kutoka kwa ndugu wa familia.
Maofisa mbalimbali wa Ubalozi wa Uingereza nchini walifika hospitalini hapo kuwajulia hali wagonjwa hao.Source:BBC News