Mwanamke
mmoja ambaye ametambulika kuwa ni mtanzania amekamatwa kwenye airport
ya Dubai
akiwa na dawa za kulevya aina ya Cocaine na alikuwa anatoka Brazil kuja Tanzania ambapo baada ya kuhojiwa na Polisi wa Dubai, kasema rafiki wa mme wake ndio alimuomba ampelekee mizigo yake nyumbani Tanzania.
Huyu mwanamke amesema alikuwa anatoka kwenye mapumziko ya miezi mitatu ambayo aliandaliwa na mume wake huko Brazil lakini anavyorudi ndiyo alipewa huo mzigo kuuleta Tanzania ambao ni dawa za kulevya aina ya cocaine zenye thamani ya zaidi ya bilioni moja nukta tatu za Dubai.
Alikamatwa wakati anajiandaa kubadilisha ndege ili kupanda inayokuja Tanzania.
Hakujatolewa taarifa nyingine zaidi ila millardayo.com inaendelea kufatilia info zaidi kwa sababu bado Mtanzania huyu anashikiliwa na polisi wa Dubai.
Hili tukio limetokea siku kadhaa baada ya mabinti wa Kitanzania kukamatwa wakiingiza dawa za kulevya kwenye nchi za Zimbabwe na Afrika Kusini wakati pia kwenye Uwanja wa ndege Dar es salaam mwanaume Mtanzania alikamatwa siku kadhaa zilizopita akiwa anasafirisha dawa za kulevya.

No comments:
Post a Comment