Nchi nzima ya Switzerland inahaha kumuomba msamaha Oprah Winfrey baada ya muuza duka na mbaguzi mmoja wa rangi huko Zurich kugoma kumuuzia mkoba kwasababu alihisi asingeweza kumudu bei yake.
Tukio hilo lilitokea mwezi uliopita baada ya Oprah kwenda Zurich kuhudhuria harusi Tina Turner.
Alienda kwenye duka la urembo la Trois Pomme ambako aliona mkoba huo uliokuwa ukiuzwa kwa $40,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 66.
Alipoomba auone, muuza duka huyo aligoma kwakuwa alikuwa na uhakika kuwa Oprah hawezi kuwa na hela hiyo.
“Nijaribu tena, nilisema ‘nataka kuuona huo, na muuza duka akasema, ‘Ohh sipendi kuumiza hisa zako’ na mi nikasema ‘Haya asante sana. Huenda upo sahihi siwezi kumudu bei.’ Na nikaondoka,” Oprah aliiambia Entertainment Tonight.
Na sasa bodi ya utalii ya Switzerland imeomba msamaha kwa niaba ya nchi nzima. Bodi hiyo pia ilimuomba msamaha Oprah Twitter.
Jana Oprah alitweet:
.@NancyODell Turns out that store clerk did me a favor. Just found out that bag was $38K!!! She was right I was NOT going to buy it.TMZ wamechombeza kwa kuandika: FYI — Oprah reportedly made $77 million dollars last year … so, suck on that racist shop assistant.
— Oprah Winfrey (@Oprah) August 9, 2013