Friday, August 23, 2013

Washiriki 20 bora wa Epiq Bongo Star Search 2013 kuingia rasmi kambini

Washiriki 20 wameingia rasmi kambini kwaajili ya shindano la Epiq Bongo Star Search 2013.
bss Rita Paulsen akizungumza na waandishi wa habari

Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Production inayoandaa shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search Rita Poulsen jana alizungumza na waandishi wa habari na kutangaza kuwaingiza washiriki wake walioingia 20 bora kambini, ambapo pia amesema litakuwa likionyeshwa na kituo cha televisheni cha TBC kila Jumapili saa tatu usiku na kurudiwa kila Jumatano saa nane mchana.
Pia alisisitiza kuwa wamepata washiriki mahiri kutoka mikoa mbalimbali kwamna mashindano ya mwaka huu yatakuwa na ushindani mkali huku akiamini watapata wasanii bora zaidi kuliko miaka iliyopita.
Bss2 Meneja TBC 1 Edna Rajab akifafanua kuhusu kituo chao cha televisheni kuonyesha mashindano ya mwaka huu ya Epiq BSS ambapo amesema ni furaha kwao kufanya kazi na BSS na kuwaahidi watazamaji kuona kipindi hicho bila matatizo yeyote
bss3 Brand Meneja wa Zantel Arnold Madale alifafanua jambo wakati shindano la Epiq BSS 2013 lilipotangaza kuwaingiza washiriki wake 20 kambini kuanza mafunzo, ambapo amesema kampuni yao imedhamiria kuboresha shindano hilo mwaka huu kwa kuongeza vitu mbalimbali
Usaili wa Epiq Bongo Star Search kwa mwaka huu umefanyika katika mikoa sita ya Arusha, Mbeya, Mwanza, Zanzibar, Dodoma na kumalizia Dar es Salaam.
Washiriki 50 walipatikana kutoka mikoa yote na wamechujwa na kubaki washiriki 20 ambao ndio watakao ingia kambini. Washiriki wanaotaka kufanya usaili kwa njia ya simu wanapaswa kupiga namba 0901551000 au watume ujumbe mfupi kwenda 15530 kupata maelezo ya namna ya kujiunga.

No comments:

Post a Comment

ShareThis