Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa kwenye mtandao wa People.com, Wentworth ameweka wazi taarifa hiyo kwenye barua aliyoandika kukataa mwaliko kuhudhuria tamasha la filamu la la kimataifa la St. Petersburg nchini Urusi.
Barua hiyo ilichapishwa kwenye mtandao wa ‘Gay and Lesbian Alliance Against Defamation’.
“Asante kwa mwaliko wenu. Kama mtu niliyefurahia kuitembelea Urusi miaka ya nyuma na ambaye nina asili kiasi ya Urusi, ingenipa furaha kusema ndio,” aliandika. “Hata hivyo, nikiwa kama shoga ni lazima niukatae.”
Aliongeza, “Ninakerwa kwa kiasi kikubwa na jinsi mashoga wanavyotendewa na serikali ya Urusi. “Hali ilivyo haikubaliki kwa namna yoyote na siwezi kushiriki kwa amani kwenye tukio linaloandaliwa na nchi ambako watu kama mimi wananyimwa haki yao ya msingi ya kuishi na kupenda kwa uwazi. Pengine, pindi mambo yakibadilika, ntakuwa huru kuchukua uamuzi tofauti.”
Barua hiyo imetokana na sheria dhidi ya ushoga iliyosainiwa na rais Vladimir Putin wa Urusi. Urusi ilipitisha sheria hiyo mwezi uliopita inayozuia mijadala ya wazi kuhusu haki na mahusiano ya jinsia moja popote pale ambapo watoto wanaweza kusikia.
Mwezi June, nchi hiyo ilianzisha sheria inayokataza kuasiliwa (adoption) kwa watoto wa Urusi na wapenzi wa jinsia moja wanaoishi katika nchi inayokubali sera za mahusiano hayo, lesbian, gay, bisexual, and transgender, LGBT.
Wentworth alijipatia umaarufu kwenye tamthilia ya Prison Break ya mwaka 2005 hadi 2009. Pia ameandika na kushiriki kutayarisha filamu ya mwaka huu iitwayo Stoker, aliyoigiza Nicole Kidman.
No comments:
Post a Comment