Hivi karibu kumeibuka matukio ya watu kadhaa kujivika kuwa na taaluma
mbalimbali ambazo si za kweli huku jeshi la polisi likifanikiwa
kuwakamata wengine wakijifanya kuwa ni maofisa wa jeshi hilo ,wengine
usalama wa taifa huku wengine wakijifanya asakri wa kikosi cha usalama
barabarani.
Afisa uhusiano wa hosptali ya Rufaa ya KCMC,Gabriel Chisseo akimwonesha anayedaiwa kujifanya daktari katika hosptali hiyo (Daktari Feki) aliyetambulika kwa jina la Alex Massawe.
Aliyejidai kuwa ni Daktari katika hosptali ya KCMC(Daktari Feki) aliyetambulika kwa jina la Alex Massawe akiwa amefungwa pingu mikononi mwake katika eneo la hosptali hiyo.
Daktari Feki Masawe akisindikizwa na baadhi ya wafanyakazi wa hosptali ya KCMC kutoka katika moja ya wodi ambayo alikuwa 'akihudumia'.
Daktari feki akiwa katika gari la polisi tayari kupelekwa kituo cha polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe
Na Dixon Busagaga, Moshi
HALI ya wasiwasi imetanda kwa baadhi ya wagonjwa wanaopatiwa matibabu
katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya mjini Moshi baada ya uongozi wa
hospitali hiyo kumkamata mtu mmoja anayedaiwa kujifanya ni
daktari wa watoto akiwa kwenye wodi ya upasuaji.
Daktari huyo feki aliyefahamika kwa jina la , Alex Sumni Massawe
alikamatwa jana majira ya saa 5 asubuhi na kuwekwa chini ya ulinzi
mkali wa makachero wa Jeshi la Polisi waliokuwa wamevalia nguo za
kiraia baada ya kukutana na mmoja wa wagonjwa ambaye alimuahidi
kumfanyia mwanae wa kiume upasuaji wa ngozi.
Kabla ya kukamatwa kwa Alex, mama mzazi wa kijana aliyekuwa akitakiwa
kufanyiwa upasuaji, Pamvelina Shirima alikutana na daktari huyo katika
baa moja maarufu mjini hapa iliyopo eneo la Dar Street (jina
limehifadhiwa) na kumtoza sh.200,000 akidai zitatumika kuharakisha
mwanae afanyiwe vipimo vya upasuaji.
Alex anadaiwa alitaka kumfanyia upasuaji kijana, Makasi Tipesa, mkazi
wa Manispaa ya Moshi ambaye amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi
kwa muda mrefu sasa.
Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya KCMC, Bw. Gabriel Chisseo alisema daktari
huyo aliwekewa mtego na uongozi wa hospitali
ya KCMC kutokana na baadhi ya wagonjwa kuripoti kutapeliwa na mmoja wa
madaktari ambaye amekuwa akijinasibu kwamba anafanya huduma hiyo
kutokana na wito alionao katika fani hiyo.
“Leo asubuhi(jana) mteja wetu ambaye amekuwa akitibiwa hapa alitapeliwa na
huyu Alex , tulimkamata akiwa wodi ya upasuaji baada ya kupokea kiasi
cha sh.200,000 kutoka kwa Pamvelina Shirima ambaye alimleta mwanae
afanyiwe upasuaji wa ngozi", alisema Chisseo.
Uongozi wa Hospitali ya KCMC umethibitisha kwamba mtu huyo
aliyekamatwa ndani ya Hospitali hiyo, si mwajiriwa wao na wala
hakukutwa na sare wala kitambulisho kinachomtambulisha kitengo chake
cha kazi.
No comments:
Post a Comment