Wednesday, September 11, 2013

The Game aanzisha mradi wa kurudisha kwa jamii kwa kutenga $1 M za kusaidia wasiojiweza na wenye shida

Rapper The Game ameingiwa na moyo wa kurudisha faida anayoipata katika biashara zake kwa kuisaidia jamii ya wasiojiweza, kwa kuanzisha mradi alioupa jina la ‘The Robin Hood Project’.
Boston Celtics v Los Angeles Lakers
Rapper Jayceon Terrell Taylor maarufu kama The Game amejiwekea lengo la
kusaidia watu wasiojiweza na wenye shida kwa kuwapa pesa zitakazofika $1,000,000 mapaka ifikapo Christmas ya mwaka huu.
The Game tayari amefungua akaunti ya Instagram atakayokuwa akiweka picha zinazoonesha matukio ya mradi huo wa kusaidia wenye shida.
Game alisema wazo la kusaidia watu wenye matatizo lilikuja baada ya siku aliyokutana na mtoto mwenye asili ya Africa huko Australia ambaye alimsimulia maisha magumu aliyokuwa nayo na familia yake na kumfanya Game apate moyo wa kumsaidia kile alichokuwa nacho.
“The other day I posted this pic of an African child I met in Australia playing outside the grocery store. His story of his families’ hardships & struggles to get away from the terror they left behind touched me so I gave him what I had on me… Which was an Australian $20 bill,”
Game aliendelea kusema baada ya siku kupita aliendelea kumkumbuka sana mtoto aliyemsaidia na kilichomuumiza zaidi ni kuwa usiku ule hakuwa na pesa zaidi za kumsaidia mtoto yule, hivyo sasa ameamua kutenga dola za Marekani 1,000,000 kwa watu atakaokutana nao popote duniani kila siku mpaka Christmas.
“As the days passed, I thought about him over & over & over & the only thing that bothered me about that night was that I didn’t have more on me to give him at that time. For some reason I just didn’t bring more money from the hotel. Since I can’t shake that feeling… I have decided to give $1,000,000 to people I come in contact with around the world everyday until Christmas,” Alisema.
Game amefungua pia akaunti twitter kwaajili ya mradi huo @therobinhoodproject

No comments:

Post a Comment

ShareThis