Sean Carter aka Jay Z na mkewe Beyonce Knowles mwezi uliopita walikamata nafasi ya kwanza katika orodha ya Forbes ya mastaa wanandoa ama wapenzi wanaoingiza pesa nyingi zaidi mwaka huu (2013) kupitia vyanzo vyao mbalimbali
Pamoja na mafanikio makubwa aliyonayo sasa Jay Z lakini amepitia maisha magumu enzi za ujana wake ikiwa ni pamoja na kuwahi kuwa muuzaji wa dawa
za kulevya.
Jay Z (43) baba wa Blue Ivy amezungumza mambo kadhaa kuhusu maisha yake ya nyuma katika jarida la Vanity Fair toleo la November.
Jay Z amefunguka kuwa aliwahi kupitia biashara ya dawa za kulevya kwa lengo la kuisaidia familia yake alipokuwa kijana.
“Tulikuwa tunaishi katika mazingira magumu, lakini mama yangu alijitahidi kumudu” alisema Jay Z. “wakati mwingine tuliweza kulipa bili ya umeme, wakati mwingine tulilipa bili ya simu, wakati mwingine gas iliisha. Hatukulala njaa, tulikuwa tunakula, lakini ilikuwa ni ile hali ya kutotaka kuaibika tunapokwenda shule , kwa kuvaa viatu vichafu au kurudia nguo kila siku”.
Jay Z (kulia) enzi za ujana wake
Katika enzi za ujana wake Jay Z amesema kuwa ‘unga’ ulikuwa kila sehemu “You could smell it in the hallways, that putrid smell; I can’t explain it, but it’s still in my mind when I think about it.” Young Jay-Z alijiingiza katika biashara ya kuuza ‘unga’ lakini amesisitiza kuwa hakuwahi kutumia dawa za kulevya.
Jigga aliendelea kusema kuwa alianza ku ’feel guilty’ baada ya kuona madhara ya dawa za kulevya kwa jamii, “Nilianza kuangalia jamii kwa ujumla, lakini mwanzo nilikuwa nawaza juu ya kuboresha hali yangu.. Niliwaza juu ya kuboresha hali yangu, nilikuwa nawaza kuhusu kununua nguo,” alisema.
Mume wa Beyonce pia ameliambia jarida hilo kuwa kuwa muuza ‘unga’ kulimfundisha ujuzi wa biashara. “Mimi najua kuhusu bajeti. Nilikuwa muuzaji wa madawa ya kulevya, ili uwe katika bisahara ya dawa za kulevya, unahitaji kujua nini unaweza kutumia….au kama unataka kufungua biashara ya kinyozi au car wash, hizo ndo zilikuwa biashara za wakati ule”. Alisema Jay Z
Jarida hilo lenye mahojiano ya Jay Z litatoka mwezi Novemba

No comments:
Post a Comment