Kama wewe ni mtoto wa kishua, huenda katika maisha yako hujawahi kuwa na gaga. Wengine wanayaita machacha na bila shaka nawe pia unalo jina lako. Gaga ni mipasuko inayotokea chini ya miguu na ni maarufu zaidi kwa watu wasiovaa viatu mara kwa mara.
Katika maisha, kila mmoja amewahi kusugua gaga kwenye jiwe si tu kwasababu anazo mguuni, bali ni njia rahisi zaidi ya kusafisha nyayo za mguu na kuziweka katika hali ya usafi. Ukweli ni kwamba gaga si vitu vya kuonesha hadharani.
Unaweza kutoswa na msichana hivihivi kama akigundua kuwa gaga ulizonazo ni nyingi kiasi cha kuweza hata kuwa makazi ya kupe na wadudu wengine.
Lakini vipi kama, katika pitapita zako ukamuona mwanamke aliyejaaliwa makalio, akiwa na kanga moja tu baada ya kutoka kuoga kwenye bafu la Kiswazi lililotengenezwa kwa mabati chakavu na huku akisugua gaga kwenye tofali? Hatari tupu.
Awamu hii, Shaa ameamua kusema na watoto wa uswazi zaidi ambao gaga kwao ni kama ‘samaki na maji’ kwa kufanya wimbo Sugua Gaga, akiwa chini ya Mkubwa na Wanae.
Swali ni? Uko tayari kusugua gaga na sauti ya Shaa?

No comments:
Post a Comment