Golikipa Juma Kaseja amesaini Mkataba wa miaka miwili na klabu ya Yanga SC kwa dau la Sh, Milioni
40 mbele ya vigogo wa Usajili wa Yanga, Abdallah Ahmed Bin Kleb na Seif Ahmed ‘Magari’ mbele ya Meneja wake, Abdulfatah Salim Saleh Ilala Dar es Salaam.
Kaseja sasa anakwenda kuungana na makipa wawili aliowahi kufanya nao kazi Simba SC, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’
Hii inakuwa mara ya pili Kaseja kusajiliwa Yanga baada ya awali kusajiliwa mwaka 2009 akitokea Simba SC ambako baada ya msimu mmoja wa mkataba wake alirudi Msimbazi.
Kaseja aliachwa Simba SC mwishoni mwa msimu kwa madai ya kiwango chake kushuka ambapo kuukosa mzunguko wa kwanza wa Ligi kuu ya bara ingawa sasa baada ya kumwaga wino Yanga anarudi kazini Januari.
Kikubwa kilichoisukuma Yanga SC kumsajili kipa huyo ni uzoefu wake katika michezo ya kimataifa na inataka inufaike naye katika Ligi ya mabingwa Afrika mwakani.
Kaseja aliibukia sekondari ya Makongo Dar es Salaam ambako aliitwa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys mwaka 2001 chini ya kocha Mnigeria Ernest Mokake aliyekuwa akisaidiwa na mzalendo Juma Matokeyo ambao wote sasa ni marehemu.
Mwaka huo huo alisajiliwa na Moro United aliyoichezea hadi mwaka 2003 alipohamia Simba alipopiga kazi hadi 2009 akaenda Yanga na kurejea mwaka mmoja baadaye ambako alifanya kazi hadi mwishoni mwa msimu uliopita alipotupiwa virago.
Pichaz na stori vimeandaliwa na bongostaz.blogspot.com ya Bin Zubeiry.
No comments:
Post a Comment