Friday, November 8, 2013

Video: Mgonjwa na madaktari waamua kucheza wimbo wa Beyonce kabla ya kuanza zoezi la upasuajiVideo: Mgonjwa na madaktari waamua kucheza wimbo wa Beyonce kabla ya kuanza zoezi la upasuaji



Kwa kawaida chumba cha upasuaji hospitalini huwa hakizoeleki, na hufanya mgonjwa kuingiwa na hofu akijua kwamba anaenda kufanyiwa upasuaji, lakini hali ilikuwa
tofauti kwa mwanamke mmoja (mgonjwa) aliyekuwa katika ratiba ya kufanyiwa upasuaji kwenye hospitali ya Mt Zion huko San Francisco, Marekani Jumanne (Nov 5), baada ya kuomba acheze wimbo wa Beyonce “Get Me Bodied” kabla ya kuanza operation
Mwanamke huyo mwenye miaka 41 aitwaye Deborah Cohan hakuonesha hali ya uoga au huzuni kama wagonjwa wengine wanaoingia ‘Theatre’, badala yake aliomba kucheza wimbo huo na kuwashawishi madaktari na wafanyakazi wengine waliokuwa kwenye chumba hicho kujumuika naye kucheza, ombi ambalo lilikubaliwa na wote wakaanza kucheza kwa furaha kama wako kwenye birthday party.
“No one was against it,” Alisema Cohan katika mahojiano na Right This Minute. “In fact, I was more nervous about how the flash mob was going to go than how the surgery was going to go.” Alisema.
Katika video hiyo mwanamke huyo ambaye tayari alikuwa amevaa nguo maalum kwaajili ya upasuaji, anaonekana akicheza kwa nguvu zote kama mtu asiyeumwa wala asiyetarajia kufanyiwa upasuaji, na baada ya wimbo kuisha wote walishangilia na kumkumbatia Deborah.
Beyonce ambaye aliiona video hiyo iliyowekwa youtube alimpa shout-out mwakamke huyo ambaye ni mama wa watoto wawili kupitia facebook “Deborah, you are awesome!” Aliandika Queen Bey.
Hata hivyo baada ya drama hiyo kazi iliendelea na upasuaji ulimalizika salama na kwa mujibu wa Aceshowbiz Cohan anaendelea ku-recover nyumbani.
Video hiyo iliyowekwa Novemba 5 mpaka sasa imetazamwa mara 3,271,845.


No comments:

Post a Comment

ShareThis