Mtangazaji wa kipindi cha ‘Wanawake Live’ kinachorushwa kupitia East Africa TV, Joyce Kiria ameamua kutoa ushauri kupitia uzoefu wake katika swala la sherehe za ndoa. Joyce ambaye hivi sasa yuko katika ndoa yake ya pili baada ya ile ya kwanza kuvunjika, ametumia jina lake kama kioo cha jamii kwa kutoa ushauri kupitia ukurasa wake wa facebook.
Joyce na mume wake baada ya kubariki ndoa yao
Hiki ndicho Joyce Kiria alichoandika baada ya tukio la kubariki ndoa yao wiki hii:
“Wacha niwape uzoefu-
1. Ndoa ya kwanza nilichangisha kama UTAMADUNI wa wengi kwenye jamii yetu…
Lakini Pamoja na michango tena mingi, tuliingia gharama zetu kubwa sana, na kama haitoshi tulikopa. Baada ya shughuli tulianza KUPIGA MIAYO YA NJAA hatuna ela na madeni juu..binafsi nilijuta sana lakini siku zote MAJUTO ni Mjukuu…(siku isiyokuwa na jina Ndoaikasambaratikia****)
2. Ndoa ya pili.(BOMANI/SERIKALINI)Mungu akanikutanisha na Henry Kilewo anaejua nini maana ya Mke, anaeniheshimu na kunitunza, anaenipenda na kunijali.
Henry akaandaa sherehe NDOGO SANA ndugu jamaa na marafiki WACHACHE sana, kwa GHARAMA ZAKE. Mume wangu Henry Hakusumbua mtu yeyote. Baada ya lile tukio wala hatukupata ile adha ya madeni na kuishiwa pesa kabisa ndani. Tukaendelea na maisha matamu kwa Upendo na Uaminifu mpaka sasa.
Ningekuwa na mawazo mgando ningefanya sherehe ya kukata na shoka.. kwanza kutetea jina langu(umaarufu mavi) na kuwazodoa waliochonga sana kwamba kanisa nitalisikia kwenye tv na redio na magazeti)
Mazoea- kwa hiyo watu wengi huwa wanafanya sherehe kubwa sana haijalishi anaanza au anaendelea ili KUWAFURAHISHA WATU WENGINE…..na hasa akiwa na jina mjini Atajitutumua hata kama uwezo hana atafanya kila awezalo aweke heshima uchwara mjini.
Mimi Joyce Kiria namshukuru Mungu amenipa Akili za Maisha siyo za darasani za kukopi na kupesti. Nilizotumia wakati ule ikala kwangu!
Ningekuwa na Akili za kukopi na kupesti NINGEFANYA PATI KUBWA SANA BILA KUCHANGISHA MTU kwa sasa namshukuru Mungu si haba uwezo wa sherehe ninao, NA HATA NINGEAMUA KUCHANGISHA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI NINGEPATA PESA NYINGI SANA KWA TAARIFA YAKO.
HITIMISHO.
TZ ndo nchi iliyobaki tunachangisha sherehe. Jirani zetu wanachangia ugonjwa na Elimu. Tukubali kubadili mitazamo yetu.
Kama unauwezo wa kufanya Sherehe fanya kwa sababu ni jambo jema sana. Usiwasumbue watu kwa michango. Haina maana hata kidogo.
Kwa sisi ambao hata uhakika wa maisha bora hatuna, tunaishi tu bora kumekucha tunamshukuru Mungu, siyo lazima tuchangishe watu, tujikite ktk kuboresha maisha yetu ili baadae tufanye sherehe bila kutegemea michango, michango ni shida kubwa sana. Kama kuna watu waliomaliza salama bila kubaki na umasikini ni wachache sana…
Au tuendelee kuchanga lakini hizo fedha zikatusaidie kwenye maisha. Wahusika wakaanzishie miradi ya kuwasaidia. Siyo kula kunywa na kucheza kwaito hapana aiseeeee…
Kwa kuwa hatukufanya Sherehe na uwezo tunao, mwakani tutawapeleka Shule watoto kadhaa wenye uhitaji kwenye jamii yetu. Yule binti aliyeshindwa kufanya mtihani wa 4m4 kule rombo, tutampeleka private kwa sababu walisema hawana uwezo huo ndo maana alikuwa tayari kuendelea kusoma wakati mtoto akiwa na wiki kadhaa toka azaliwe, wale watoto 3 wa Stela aliyekatwa mkono huko dodoma kama unawakumbuka, watoto 2 wa Gati Chacha aliyekatwa mguu huko Tarime Mara n.k
Tuchangie maendeleo tuachane na sherehe….Kenya wameweza kwa nini TZ tushindwe?!
Wanangu nitawasihi sana wasifanye SHEREHE bali wasaidie wengine au waanzishe miradi na kama wana uwezo basi wafanye bila kuathiri uchumi wao na wasisumbue watu.”

No comments:
Post a Comment