Mwimbaji wa
THT Linah Sanga amekanusha taarifa zilizosambazwa kupitia mtandao wa kijamii wa
facebook na mitaani kuwa amebakwa na rapper Kimbunga.
Akiongea na
mtandao wa Bongo5 Linah ameshangazwa na kusikitishwa na taarifa hizo
zilizoonekana pia kupitia ukurasa wa facebook wa rapper wa Kikosi cha Mizinga
KalAPina jana kupitia akaunti yenye jina ‘Kala Pina Kikosi cha Mizinga’.
“mtoto kimbunga amechamba ana leta usela mavi mambo ya
kizamani hivi yupo chini ya ulinzi osterbay police kwa kosa la kumbaka msanii
lina.” Aliandika Kala Pina.
Linah amesema alipigiwa simu na watu
wake wa karibu wakimuuliza kuhusu taarifa hizo akiwemo Ditto, Barnaba na Amini.
Amesema ameshangazwa na taarifa hizo
ambazo na yeye ameambiwa zimeandikwa na Kala Pina lakini hakutaka kujipa stress
kwa kuwa kuna kazi anaifanya asije akaiharibu na kwamba vitu vingine kama hivyo
ni vya kuvipotezea tu, lakini hakupendezwa kabisa na taarifa hizo.
“Kiukweli sijapenda, yaani bora mtu
anizushie kitu kingine chochote lakini si suala hili hapo, si suala zuri.” Alisema
Linah.
Aliongeza kuwa jumamosi usiku
alikuwa ametoka na boyfriend wake kwenda kuangalia cinema na hakuna kitu
kingine kilichotokea kwa hiyo hafahamu kabisa taarifa hizo zimetokea wapi na
wala hata huyo Kimbunga yeye hamjui.
“Sasa sielewi huko kubakwa nimebakwa
saa ngapi na nilikuwa na boyfriend wangu, labda yeye ndo kanibaka. Maana mtu
anaeniambia amenibaka kimbunga, huyo Kimbunga hata simjui namsikia tu. Nashindwa
kuelewa, kwa nini mtu azushe kitu kama hicho yaani ndo nataka kujua source ni
nini.” Alisema Linah.
“ Niko fine yaani, kwa sababu
naelewa it’s not true, lakini nafikiria huyo mtu mpaka kaamua kunifanyia kitu
kama hicho, nimemkosea nini au kuna kitu gani yaani hicho ndicho kinaniumiza
kichwa.”
Kwa mujibu wa mtandao huo ulimtafuta
Kala Pina kutaka kujua kulikoni, lakini yeye alisema habari hizo zipo na
zimeenea katika maeneo mengi ya Kinondoni na kwamba watu wanaendelea kudai kuwa habari hizo ni za
kweli.
No comments:
Post a Comment