Friday, July 19, 2013

Oprah Winfrey Avutiwa na Tanzania: arejea Marekani jana, asema atarudi tena Tanzania ‘soon’

 Malkia wa talk show duniani, Oprah Winfrey jana ameondoka nchini Tanzania kurejea kwao Marekani baada ya kukaa kwa siku kadhaa kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti alikoenda kwa ziara binafsi.
BDPodYjCQAEnI2Q
Tajiri namba 107 nchini Marekani (kwa mujibu wa Forbes), Paul Tudor Jones II, mwanzilishi wa kampuni ya Tudor Investment Corporation ndiye aliyekuwa mwenyeji wake nchini.
Jones ambaye ana utajiri ufikao dola bilioni 3.3 ambao unamfanya pia awe tajiri wa 330 duniani, ni mwekezaji mkubwa huko Serengeti. Tajiri huyo ndiye mmiliki wa hoteli za kifahari mbugani huko za Singita Grumeti Reserves (SGR) ambazo zinajumuisha hoteli za , Sasakwa, Farufaru, Sabora Tented Camp na Singita Explore Mobile Camp.

Oprah aliyetua Serengeti weekend iliyopita, alikuwa anatokea nchini Hispania na alipokelewa na naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Kwa mujibu wa Mheshimiwa Nyalandu, Oprah anapanga kuja tena nchini Tanzania muda si mrefu lakini haijulikani atakuja kwa madhumuni yapi.

Amesema Oprah ameufurahia ujio wake nchini na kwamba Tanzania imepiga hatua kubwa katika sekta ya Utalii.
Kuna uwezekano mkubwa kuwa Oprah anaweza kuwa amevutiwa na fursa za uwekezaji nchini hususan Serengeti.

No comments:

Post a Comment

ShareThis