Sunday, September 15, 2013

KAMATA FURSA TWENDZETU KWA VIJANA IMEFANYIKA MKOANI MOROGORO LEO.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mwansiti Almasi,akifafanua namna anavyonufaika na huduma za NSSF,mara tu walipojiunga kupitia
kundi lao la Lekadutigite,ndani ya semina ya fursa twendzetu iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Katema Hall,Midland hotel mkoani Morogoro mapema leo asubuhi.
 Mbunifu wa mavazi kutoka mkoani Morogoro,ambaye pia ni mjasiliamali aliyejitambulisha kwa jina la Diana Magessa akionesha mbele ya washiriki wa semina ya Fursa kwa Vijana (hawapo pichani) baadhi nguo zake alizozidizaini kwa ubunifu wake.

Meneja huduma wa Wajasiliamali-Zantel akizungumza mbele ya sehemu ya wakazi wa Morogoro waliojitokeza kwenye semina ya Kamata fursa twendzetu,kuhusiana na fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya kampuni hiyo,Semina hiyo iliofanyika ndani ya ukumbi wa Katema Hall,Midland hotel mkoani Morogoro mapema leo asubuhi iliwakutanisha wadau mbalimbali.Semina ya kamata fursa twendzetu inaratabiwa na Clouds Media Group,ambapo kwa sasa imekwishafanyika ndani ya mikoa zaidi ya nane,ikiwemo Kigoma,Singida,Tabora,Dodoma,Mtwara,Mbeya,Morogoro pamoja na Iringa.
 Mkali wa kughani Mashairi,Mrisho Mpoto akizungumza na wakazi wa Morogoro waliojitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya fursa twendzetu ndani ya ndani ya ukumbi wa Katema Hall,Midland hotel mkoani Morogoro mapema leo asubuhi.
 Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji, Ruge Mutahaba akifunga semina ya kamata Fursa twendzetu kwa vijana, iliyofanyika mapema leo mkoani Morogoro.


No comments:

Post a Comment

ShareThis