Wednesday, September 4, 2013

Mfanyabiashara wa Sweden anunua ndege aina ya Boeing 747 na kuigeuza kuwa Hostel! (Picha)

Mfanyabiashara Oscar Divs wa Sweden aliiona fursa na kuamua kuinunua ndege aina ya Boeing 747-200 na kuamua kuigeuza kuwa ‘Jumbo hostel’ iliyopo eneo la uwanja wa ndege wa Arlanda, karibia na jiji la Stockholm, Sweden.
ndege-11
Ndege hiyo Boeing 747-200 iliyokuwa na uwezo wa kubeba abiria 450 sasa imegeuka kuwa
hostel yenye vyumba 27 vyote vikiwa na Wi-Fi pamoja na flatscreen TVs.
ndege-6
Hostel hiyo ya kwenye ndege ina luxurious cockpit suite ambayo ina view nzuri ya uwanja huo wa ndege, na ina uwezo wa kutumika kwaajili ya mikutano na ipo wazi saa 24 katika siku 7 za wiki kwaajili ya wageni.
ndege-5
Bei za hostel hiyo kwa usiku mmoja ni kuanzia USD 65 kwa chumba cha mtu mmoja na USD 264 kwaajili ya ‘exclusive pilot’s suite’.
Ndege hiyo 747-200 ya mwaka 1976 mara ya mwisho ilikuwa ikimilikiwa na kampuni ya Transjet ya Sweeden ambayo ilifilisika 2002.
ndege-10
ndege-1
ndege-2
ndege-3
ndege-4
ndege-7
ndege-8
ndege-9


No comments:

Post a Comment

ShareThis