Thursday, September 5, 2013

Mwanamke wa Nigeria akamatwa JNIA na kete 99 za dawa za kulevya alizodai amenunua Magomeni, DSM

Vifaa vipya vya ukaguzi vilivyofungwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA) hivi karibuni kufuatia juhudi za waziri wa uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe za kupambana na biashara hiyo haramu vimeanza kuzaa matunda, baada ya mwanamke raia wa Nigeria kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana, akiwa na kete 99 za dawa za kulevya.
dawa3


dawa9
Akizungumza na gazeti la Mwananchi , Meneja Usalama wa uwanja huo, Clemence Jingu, alisema mtuhumiwa alikamatwa Jana (September 4) saa 8:00 mchana akiwa na kete 99 za dawa za kulevya akiwa amezificha katika makopo ya poda na mafuta.
“Kete hazijajulikana ni za aina gani, kwa sasa tunafanyika utaratibu wa kutambua aina yake,” alisema.
dawa3 Anthonia baada ya kukamatwa

“Kwa sasa hapa JNIA kuna mitambo ya kisasa ya kuweza kuwabaini wanaopitisha dawa hizi, tulimkamata akiwa na kete 99, kati ya hizo kete 30 alikuwa ameweka katika kopo la mafuta ya nywele, kete nyingine alikuwa ameweka katika kopo la poda za watoto,” alisema.

dawa5 Akizitoa kete hizo alizokuwa amezificha kwenye makopo ya poda
Alisema Anthonia Ojo (25) raia huyo wa Nigeria alikuwa akielekea Roma, Italia kupitia Paris, Ufaransa kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.
dawa4  
Hati yake ya kusafiria
“Baada ya kumhoji ametueleza kuwa dawa hizo alizinunua maeneo ya Magomeni, kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi na mahojiano zaidi,” alisema.


dawa11

Alisema kuwa binti huyo aliingia nchini Agosti 30mwaka huu, akitokea nchini Nigeria.
Source: Mwananchi, Picha: Rober Okanda

No comments:

Post a Comment

ShareThis