Thursday, September 19, 2013

Picha: Staa wa filamu wa Ghana, Van Vicker atua Dar kushoot movie

Staa wa filamu wa nchini Ghana, Van Vicker wiki hii ametua nchini nchini kwa mwaliko wa kuja kuigiza filamu. Vicker ambaye ni kipenzi cha akinadada ataigiza kwenye filamu moja na Hashim Kambi.
d3a61884203411e38d1d22000aeb11b8_7 Van Vicker akiwa kwenye Mgahawa wa Akemi, Dar es Salaam

Kupitia Facebook, Kambi amefafanua kuhusu ujio wa staa huyo:
“Tangu jana nimepata simu nyingi kuulizwa kama yanayozungumzwa ni kweli, napenda nitamke kwa furaha sana kuwa yule muigizaji nyota wa afrika magharibi anayetokea ghana yuko hapa tanzania kwa kufanya kazi na mimi kama ambavyo yeye aliniita ghana mwezi wa 2. Hivi tuko location tunaendelea na shooting na mtaziona picha zake muda si mrefu. Nimetimiza ahadi yangu ya kuhakikisha kuwa namleta hapa Bongo na ana furaha sana. Wengine ambao wanashiriki katika movie hii ninayocheza na Van Vicker ni Irene Paul, Slim Omari, Sandra na Weru Sengo. Natumaini ndugu na marafiki zangu nanyi mtaungana nami katika kumuomba zaidi mwenyezi Mungu.”
18d8c6c2203511e3849f22000aeb126c_7 Vicker alipiga picha hii ya mandhari ya Dar na kupost kwenye Instagram
cf015dfe20f511e3ab4322000a1fa430_7 Lulu akiwa na Van Vicker
van

No comments:

Post a Comment

ShareThis