Six Degrees South ipo eneo la mji mkongwe na inawapa wageni utulivu wa hali ya juu ili kuwawezesha kupumzika na kujichanganya. Ukichanganya mazingira ya utulivu na na huduma ya bure ya mtandao wa internet,
Picha zaidi bonyeza Read More.......
Wakati
upepo mzuri wa kipindi cha joto kutoka bahari ya Hindi ukipuliza,
uzinduzi wa mgahawa mjini Zanzibar, Six Degrees South, ulikuwa hauna
mfano! Huku kukiwa na fataki za ndani, chupa za Moet zikifunguliwa kwa
madaha usiku kucha mpaka mida ya usubuhi, uzinduzi wa Six Degrees South
uliwaacha wengi mjini Zanzibar wamepigwa na butwa wakiwa hawana la
kusema.
Huku
Wanzibari wengi wakiwa wana hamu ya mgahawa kama huu, muundo wa mgahawa
huu wa kisasa wenye ghorofa tatu umedhihirisha hadhi yake ya kuwa na
eneo la nyama choma na baa ya mvinyo. Kuanzia ordha ya vyakula vya moto
vya asubuhi mpaka mchanganyiko murua wa vyakula vya siku nzima na
vitafunio vidogo vidogo, sehemu hii imeinua viwango vya biashara ya
migahawa mjini Zanzibar na kuifikisha juu kabisa.
Six
Degrees South ipo eneo la mji mkongwe na inawapa wageni utulivu wa hali
ya juu ili kuwawezesha kupumzika na kujichanganya. Ukichanganya
mazingira ya utulivu na na huduma ya bure ya mtandao wa internet, sehemu
hii inamfaa mtu yoyote kupata kinywaji anachopendelea na vitafunwa.
Mgahawa una vibaraza kwenye ghorofa tatu vyenye eneo kubwa kwa ajili ya
wageni kutazama jua likizima kwenye mandhari ya Bahari ya Hindi.
Vyakula
kutoka mataifa mbalimbali pia vitapikana kwa ya wateja wenye ladha na
uwezo tofauti. Orodha ya chakula iliyoandaliwa na Mpishi Mkuu kutoka
Afrika Kusini, Louise Serfontein, inatoa fursa kwa watu kutoka bara na
visiwani kufuruhia chakula. Six Degrees South inajisifia kwa kuwa na
viwango vya hali ya juu ya utoaji huduma wakati wakiwaridhisha wateja
kwa chakula na mandhari nzuri.
Huku
wakiwa na orodha ya mivinyo zaidi ya 80 ambayo mteja anaweza kunywa kwa
glasi au chupa, Six Degrees South inatoa fursa nzuri ya kunywa, kula na
kufanya matembezi wakati mwezi ukiangaza kwenye bahari.
Sehemu yenye kutoa ukarimu wa hali ya juu, Six Degrees South ni sehemu ambayo kila mtu anatakiwa kutembelea.
No comments:
Post a Comment