Sunday, August 11, 2013

Kifafa alichopata Chris Brown kilisababishwa na msongo mkubwa wa mawazo

Imebainika kuwa kifafa alichopata Chris Brown jana kilisabishwa na stress zinazomwandama kutokana na jinsi vyombo vya habari vinavyomwandika vibaya.



chris brown pink dolphin 071112

 

Jana TMZ waliripoti kuwa kitengo cha zima moto cha Los Angeles kilienda kwenye studio ya kurekodia muziki baada ya mtu mmoja kupiga 911 na kudai kuwa Chris alikuwa amepatwa na kifafa. Hata hivyo Chris aligoma kutibiwa.
Mwakilishi wa Chris anasema kifafa hicho kilisababishwa na uchovu mkali na msongo mkubwa wa mawazo na vyote vikitokana na kesi zinazomkabili na jinsi anavyoandikwa vibaya.
Baadaye Chris alitweet:
‘Hawatakupenda hadi uwe kumbukumbu’

ShareThis