Life Style

Vitu ambavyo kila mwanamke anabidi avijue.


Kama upo ndani ya ndoa au ndani ya mahusiano,au kama bado unampango wakuingia katika mahusiano,ukiwa kama mwanamke unayetaka siku moja rafiki wako wakiume akuoe,au kama upo ndani ya ndoa asiweze kuchepuka,ushauri wa bure huu hapa,yajue haya kuhusu mwanaume na tabia za wanaume wengi,ili kuweza kudumu katika mahusiano yako kwa muda mrefu.
Kuwa rafiki yake wa karibu.
black-couple-in-bed
Kila mwanaume anataka kuoa rafiki yake wa kike,anaweza kuwa na wanawake wengi wazuri tu,ila mwisho wa siku ndo pale unajiuliza mbona kaoa mwanamke wa kawaida tu ,hata siyo mzuri sana ukilinganisha na girlfriend zake wa zamani,ila yule ambaye wanaweza kucheka wote, wakanywa wote,wakumfichia siri zake,ambaye kweli anaweza kujiachia mbele yake na kufanya all the crazy things na wewe,basi kuna asilimia mia kuwa hawezi kukuacha,wanaume wengi wanaishia kuoa wanawake wa haina hii,kwa sababu wanajua kuwa mbeleni,mapenzi huwa yanaweza kuisha,ila kinachobakia,ni jinsi gani mnaweza kufaana hata kama mapenzi yakipungua.
Mkumbushe ni nini alichonacho.
igcgzy3a
Kama unaona kuwa imefika wakati kuwa kila uongeacho mbele ya mpenzi wako, unaona kama unamsumbua,hakusikilizi tena kama zamani na kum-boa,inabidi uanze kufikiria njia mpya ya kumuingilia,mara nyingi hata wanaume nao wanataka kusikia kuwa unawaambia unampenda,uko kwa ajili yake,hii itamkumbusha mambo mengi wakati mapenzi yenu yalivyokuwa bado machanga,nakumkumbusha jinsi gani analivyowahi kukupenda na anavyokupenda.
Wanaume nao huwa wanahitaji muda wa peke yao.
Black-Couple-Arguing-pointing
Kama humpi boyfriend wako hata lisaa limoja tu ya yeye kuwa mwenyewe,anapofika nyumbani ,huu ndo mwanzo wa kuanza kumuona anachelewa kuja nyumbani,nakumkuta anapitia baa na ndio mwanzo wa kuanza kumuona ananza kutafuta wengine,inabidi humpe some space ,siyo lazima aku-text kila dakika ili kuonyesha kuwa anakupenda au kumlalamikia kila asipokupigia baada ya muda Fulani.hii inamkosesha amani sana mwanaume tena baada ya kutoka kazini,bila kujua hata huko kazini yamemkuta nini,au siku yake ilikuaje,unakuta wanawake wengi wataanza kuongea na kuongeza matatizo yao.

 ____________________________________

Utafiti: Wapenzi kulala vitanda tofauti usiku husaidia kuimarisha mapenzi yao

Swala la kulala vitanda tofauti kwa wapenzi linaweza kuwa na tafsiri mbaya kwa wapendanao lakini utafiti wa hivi karibuni umeonesha kuwa matokeo yake yana faida zaidi ya hasara katika mahusiano.
couples separate beds-1
Utafiti uliofanywa Ryerson University huko Toronto, Canada, umeonesha kuwa kati ya asilimia 30 na 40 ya wanandoa hulala vitanda tofauti usiku, na wataalamu wanasema kujitenga wakati wa kulala kunaweza kuwa na faida zaidi katika kusaidia kuimarisha uhusiano zaidi ya madhara yake.
Colleen Carney, mwandishi wa utafiti huo aliiambia CBS kuwa, wanandoa (couples) wanaolala pamoja huwa hawapati kiwango cha usingizi kinachotakiwa. Badala yake hua wanajikuta wanaamshana mara kwa mara kwa milio mbalimbali (mikoromo) na kujigeuza mara kwa mara.
couples separate beds-2
Aliendelea kusema kuwa wapenzi wanapaswa wafikirie juu ya kulala tofauti kwa faida ya kupata mapumziko bora ya usiku na kuboresha mahusiano.
Carney pia alizungumzia dhana iliyozoeleka kuwa wanandoa au wapenzi wakilala tofauti basi wanakuwa wamegombana kwa kusema kuwa ‘Watu wanaweza kuwa na uhusiano mzuri sana na wa kuridhisha kwa kulala mbali mbali, watu wengine wanaweza hata kuwa wanaelekea kupeana talaka lakini kwa kulala tofauti inaweza kusaidia wakarudisha mapenzi yao’.
Alitoa mfano wa wapenzi wa Canada walioishi kwa kulala vitanda tofauti kwa miaka 14 na mpaka sasa ni wanandoa wenye furaha.

_________________________________________________________________________

Utafiti: Mama wa nyumbani wana furaha zaidi kuliko wanaofanya kazi

Utafiti uliofanywa nchini Uingereza umebaini kuwa akina mama wanaokaa nyumbani huonekana kuona maisha kuwa na thamani zaidi kuliko wale wanaoenda kazini.
600-00934319
Wanawake hao huepukana na hisia za kuboreka, kuchanganyikiwa ama hisia za kutojiona hawana thamani.
Utafiti huo ulibaini pia kuwa watu waliooa/olewa wameridhika zaidi kuliko wale wanaoishi pamoja bila kufunga ndoa na wana furaha zaidi kuliko wale walio single ama waliotarakiana.
shamim-weddinmg-8
Utafiti huo ulitokana na survey iliyofanywa kwa watu takriban 165,000 walioulizwa namna walivyoridhika, wanavyohisi uthamani, furaha ama wasiwasi katika maisha yao.

________________________________________________________________________

Ushauri toka kwa wazoefu kwa mabinti wote ambao bado hawajaolewa


jumping-the-broom

Ndoto ya wasichana wengi ni siku moja kuja kuolewa. Mungu ametuahidi baraka zake nyingi ikiwamo baraka ya ndoa hivyo haupaswi kukaa na kusubiri hadi upate mchumba ndio uanze maandalizi yakupasa kuanza kujiandaa kuwa mke. Mungu amekuandalia mume mwema hivyo unapaswa kujiandaa mapema ili ndoa yako iwe bora.


1. Omba kwa ajili ya mume wako Wasichana wengi wanaomba ili waweze kuolewa, hiyo ni sawa kabisa lakini jambo la kwanza kabisa inabidi uombe kwa ajili ya mume wako ambaye Mungu anaenda kukupatia. Anza mapema kuomba kwa ajili ya mume ambaye Mungu anaenda kukupatia. Omba kwa ajili ya maisha yake ya kiroho, uwezo wake kusimamia na kuitunza familia na maisha yake kwa ujumla. Usisubiri hadi uolewe ndipo uanze kuombea umoja katika ndoa yenu, anza sasa na pia kumbuka kuomba kwa ajili yako ili uwe mke mwema.

2. Jiandae Familia yako unayoishi nayo ndio hasa sehemu yako ya kujiandaa kuishi na mume wako. Unapaswa kujifunza kuanzia sasa kuishi vizuri na watu wa familia yako, hutaweza kuishi vizuri na mume wako kama sasa unashindwa kuishi vizuri na ndugu na jamaa zako. Waonyeshe upendo, huruma na kujali na kwa kufanya hivi utakuwa umejijengea tabia ambayo utakuwa nayo kwa watu wote na mumeo pia. Unaposhindwa kukaa vizuri na watu wako wa karibu kama familia vivyo hivyo hautaweza kukaa vizuri na mume wako, ndoa haimbadilishi mtu bali inakuonyesha uhalisia wako. Jinsi ulivyo unapokuwa nyumbani kwenu ndivyo ulivyo.

3. Omba uweze kutambua hila za shetani Sababu ya uhitaji wa kuolewa ulionao inaweza kuwa ngumu kugundua kama mtu anayetaka kukuoa hajatoka kwa Mungu. Sio kila nayesema Bwana asifiwe ni kweli ameokoka maana wengine wapo ili wapate wake wazuri, ndio maana ni muhimu sana kuomba uongozi wa Mungu ili uweze kujua nani hasa ametoka kwa Mungu. Pia inawezekana akawa ameokoka lakini akawa sio mume ambaye Mungu amekuandalia hivyo ni muhimu sana kuomba kwa ajili ya uongozi wa Mungu katika muda huu wa muhimu katika maisha yako.

4. Tulia mbele za Mungu Filipi 4:6 Msifadhaike juu ya jambo lo lote; lakini katika kila jambo mjulisheni Mungu haja zenu, kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru Mungu analifahamu hitaji lako na muhimu zaidi anakujua na kukupenda, hajakusahau maana hawezi kukusahau na anakuwazia yaliyo mema. Ebrania 13:5b kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, “Sita kupungukia kamwe wala sitakuacha” Yeremia 29:11 Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu,’’ asema BWANA. “Ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru,ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo”. Usikate tamaa, mume wako yupo na atakuja kwa wakati wa Bwana.

___________________________________________________________________________________

Mambo ya kuzingatia unapomkosea mpenzi wako



Mambo ya kuzingatia unapomkosea mpenzi wako 
Kukosea katika maisha ya binadamu ni kawaida. Ni sehemu ya maisha yake. Tena inaaminika kwamba, kukosea ni kujifunza, maana kosa utakalofanya leo ni funzo la kesho. Hii ipo pia hata katika uhusiano na wapenzi wetu, mara kadha wa kadha tumejikwaa na kuwakosea.
Hakuna cha ajabu. Ni kawaida kabisa, lakini jambo la msingi hapo ni kwa namna gani tunajifunza kupitia makosa. Ni kwa jinsi gani tunamaliza tofauti hizo. Maana unaweza kuwa hodari wa kukosea au ukawa bingwa wa kusamehe, lakini wimbo huo ukaendelea kubaki hivyo hivyo kila siku.

Lakini pia, wapo ambao kwa bahati mbaya, bila matarajio yao, wanajikuta wakiwa wamewaudhi wapenzi wao. Ni bahati mbaya na yawezekana kabisa wanaumia sana mioyoni mwao, lakini wakashindwa jinsi ya kumaliza tatizo hilo katika penzi lake.
Siku zote mkosewa hukosa raha, hupoteza hamu ya kukutana na mpenzi wake lakini kubwa zaidi, hushusha thamani ya mapenzi yake kwako. Lakini mkosewa huyo huyo, akioneshwa kwamba makosa yaliyofanyika hayakuwa ya makusudi na kutumia njia bora za kufikisha hisia zako kwake, hujisikia amani na hali yake kurejea kawaida.

Yawezekana ukawa upo katika kipindi cha matatizo na mpenzi wako na hujui jinsi ya kuweka mambo sawa. Wakati mwingine huna tatizo, lakini kwasababu upo kwenye uhusiano basi si ajabu mambo kwenda mrama siku moja. Leo hii, tutaangalia mambo ya kuzingatia unapomkosea mpenzi wako.

TAFAKARI UKUBWA WA KOSA
Hapa tayari umeshagundua kwamba umemkosea mpenzi wako na ni kweli kwamba unaumizwa sana na kosa lako, lakini kwa sababu hujamwambia chochote mwenzi wako, naye hana raha na wewe. Hana amani ya moyo.

Hapa unashauriwa kutulia na kutafakari ukubwa wa tatizo. Kufahamu ukubwa wa tatizo kutakupa muongozo mzuri sana wa jinsi ya kutatua tatizo hilo. Angalia ulimfanyia nini na kwa kiwango gani.

JUTIA KWA MOYO
Hii ni kwa ajili yako wewe mwenyewe. Kutakuwa hakuna maana yoyote ya kuomba msamaha wa kinafiki au kuomba msamaha ili kumaliza mambo, kama msamaha wako haujatoka moyoni.

Ukiwa peke yako, jiaminishe kwamba umekosea na kwa hakika unahitaji kusamehewa. Jutia ndani ya moyo wako, kwa dhati kabisa ukiwa na ahadi kwamba hutarudia tena. Hili ni zoezi la Kisaikolojia, ambalo litakusaidia baadaye wakati ukikutana na mpenzi wako kwa ajili ya kuomba msamaha.

MWELEZE UKWELI
Omba kukutana naye. Yawezekana hata mawasiliano si mazuri sana, lakini hapa jitahidi kumuomba mkutane, ikishindikana, tumia mtu wake wa karibu. Omba kutoka naye kwa ajili ya kuzungumza.

Mweleze ukweli wa kosa lako, onesha jinsi linavyokutesa na kukusumbua. Usijaribu kuongea uongo wowote katika suala hili. Kuwa mkweli, jutia kwa moyo, aone majuto yako usoni mwako.
Mwambie jinsi unavyoteseka na jinsi msivyo katika maelewano mazuri. Kauli yako ya ukweli, hisia zako wakati wa kuzungumza, ndivyo vitakavyokuweka katika mazingira mazuri ya kuweka mambo sawa.

AHIDI KUTORUDIA
Bila shaka, kama utakuwa umefuata taratibu zote hizo kwa umakini, uwezekano wa kusamehewa ni mkubwa sana. Hili ndilo matarajio yangu, naamini hata wewe pia, lakini ili msamaha huo ukamilike, mhakikishie mpenzi wako kuwa hutarudia tena.

Mwambie kwa kumaanisha, kwamba umegundua udhaifu wako na haupo tayari kumfanya tena asiwe na furaha tena. Hakuna uchawi ni maneno tu!

MFANYIE KITU MAALUM
Hapa unatakiwa kufanya kitu maalum kwa ajili ya mpenzi, ukionesha kwamba umekubaliana na msamaha wake na mambo yameisha. Kitu utakachokifanya hapa utalinganisha na ukubwa wa kosa kama nilivyosema awali.

Unaweza kutoka naye na kwenda kulala naye hotelini, ukihakikisha unampa mahaba mazito kama shukrani kwake. Yapo mengi ambayo unaweza kuyafanya kulingana na uwezo wako kifedha. Fanya vyovyote ili kosa
Stink like a celebrity

Stink like a celebrity

Want to smell like a celebrity? Well good news – there are over 500 celebrity fragrances released every year, according to research first NPD.

And it’s big business with celebrity fragrances pulling in 1.3b. But not all are as sweet as they sound – in fact, according to Dina Fierro of Eye4Style.com, “very few celebs have done fragrance the right way.”

“They only work when the scent is true to who the celebrity is,” added Jeannine Morris of Beauty SweetSpot.com. “The fragrance should reflect the brand and personality of the celebrity, from the notes to the packaging.” 




There are plenty that do succeed – Lady Gaga’s Fame has been a runaway success with her little monsters, Halle Berries perfumes are universally praised, Sarah Jessica Parker’s Lovely is still a favourite, and trail blazer Elizabeth Taylor’s White Diamonds is still on shelves and selling today.

One such perfume is Justin Bieber’s Someday, which was released in 2011 and said he chose to design a perfume for his female fans because the way a girl smells is “important to a guy”.

I have such a deep connection with my fans, so creating a fragrance that I personally love is another way I can bring them closer to my world.”

“They really let me take the lead on the entire project, because I know my fans better than anyone – from working with the team on the development of the fragrance itself to helping to design the bottle and packaging.”

And despite the singer’s detractors, experts gave the scent a thumbs up and it raked in more than $3m in the first three weeks, topping the previous record set by Beyonce Knowles Heat perfume in 2010, according to the Belfast Telegraph.

Riding on his previous success, Justin has just released the The Key which he says, “will unlock a personal side of me they’ve never seen before, bringing us closer than ever.”

But while Justin’s scent may have worked, there are plenty of others that didn’t!

Here are the stinkiest celeb perfumes that might be best left for toilet spray…


Stink like a celebrity - worst fragrances

Lady Gaga - The Fame

Lady Gaga - The Fame

The smell of blood, sex, semen and even Gaga’s DNA hyped the release of her perfume, and even though Little Monsters couldn’t wait to snap it up, we think it smells a little bit like those scratch and sniff strawberry stickers you stuck on your maths test book when you were a kid. Other reviewers said they were underwhelmed after all the hype as it wasn’t as ‘unique’ as they’d hoped.

ShareThis