Joseph Haule aka Profesa Jay ameiambia Bongo5 kuwa kila kitu kimekamilika upande wa vifaa vya
studio ikiwa ni pamoja na ‘setup’ iliyofanywa na producer Duke lakini bado haijaanza rasmi kuifanya kazi.
“Nadhani wiki hii kila kitu kitakuwa kwenye pipeline sema kuna taratibu za kisheria ndio bado nazishughulikia lakini soon itaanza”. Alisema Jay.
Professa Jay ameahidi kutaja jina la producer atakayemfanyia kazi pamoja na jina la studio pale taratibu zote zitakapokamilika na kuwa tayari kuifungua rasmi.
Jay anakua miongoni mwa wasanii wanaomiliki studio zao za kurekodi Muziki Tanzania ambao ni pamoja na Dully Sykes, Quick Rocker, Mb Dogg, Benjamin wa Mambo Jambo, Juma Nature, Kikosi cha mizinga na wengine.
No comments:
Post a Comment