Friday, July 26, 2013

Jay-Z aripotiwa kumpa ushauri Kanye West kuhusu hali ya kuwa baba na kuwa mfano kwa mwanae




Wanasema a Friend in need is a friend in deed, hiki ndicho kinaonekana kutokea kwa maswaiba wa ‘Watch the Throne’  ambapo Jay-Z ambae ni baba wa mtoto mwenye umri wa miezi 18 ameona swaiba wake Kanye West ambae ni baba wa mtoto mwenye umri wa mwezi  mmoja na wiki kadhaa anahitaji ushauri ili atulie na mwanae na kuwa baba bora.



Chanzo kimoja kimeliambia gazeti la The Daily kuwa Jay Z anajaribu kumpa ushauri rafiki yake ili atulie na asifuatilie sana kinachomtokea katika public bali afocus katika swala la  kuwa baba wa mwanae North West. 


“Jay’s been giving him a little bit of coaching on staying calm in public. He’s told him he should zone out, not focus on what’s happening around him and instead enjoy what he’s got.”



Chanzo hicho kiliongeza kuwa Jay Z anajaribu kumkumbusha Kanye West  kuwa sasa hivi  ni baba wa mtoto wa kike na anapaswa kuwa mfano mzuri kwa mwanae.



Ripoti hizi zinakuja baada ya Kanye West kuwa katika msala wa kupambana na paparazzi kwa vipindi tofauti, lakini pia ana kesi ya kujibu akituhumiwa kuhusika katika jaribio la unyang’anyi (attempted robbery) baada ya kujaribu kumnyang’anya camera paparazzi mmoja katika uwanja wa ndege wa LAX.



Jay-Z aripotiwa kumpa ushauri Kanye West kuhusu hali ya kuwa baba na kuwa mfano kwa mwanae.

No comments:

Post a Comment

ShareThis