Friday, August 16, 2013

Aki Na Ukwa wakanusha habari zilizoenea za wao kupata Ajali.

 
Akizungumza na mtandao mmoja nchini humo Aki alithibitisha kuwa hajapata ajali ya gari kama habari zilivyovumisha na baadhi ya watu na…

Staa wa filamu za Kinageria Chinedu Ikedieze‘Aki’amekanusha kupata ajali yeye na swahiba wake Iheme Osita ‘Ukwa au Pawpaw’ katika barabara ya Niger nchini humo.

Habari za kupata ajali kwa mastaa hao zilitapakaa kwenye mtandao wa facebook kuwa wamepata ajali mbaya na kwamba wamekimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Akizungumza na mtandao mmoja nchini humo Aki alithibitisha kuwa hajapata ajali ya gari kama habari zilivyovumisha na baadhi ya watu na kusema kuwa kwanini baathi ya watu wanapenda kuwaombea mabaya binadamu wenzao kwa kuvumisha habari mabaya kama hizo.
‘Niko poa sijapata ajali hizo ni habari za uongo"alisema Aki.

No comments:

Post a Comment

ShareThis