Ikiwa imefika siku ya 63 kwenye jumba la
Big brother, Kenya ilishuhudia kumpoteza mshiriki wao wa pili Annabel
kwenye jumba la Big brother baada ya Hudda kutoka long time. Baada ya
kufika Kenya kwenye mkutano na waandishi wa habari, Annabel alisisitiza
kwamba anachojivunia kwenye jumba la Big brother ni kutokufanya kitu
chochote kilicholeta utata kwa watazamaji.Kikubwa kilichomfanya yeye
kuishi vile ni background yake ya dini iliyomsaidia kutofautisha maisha
yake binafsi na ya kwenye mchezo wa Big brother. Annabel mwenye miaka 24
ni mwanafunzi na mbunifu wa mitindo, alikuwa ni rafiki mkubwa wa Nando
ndani ya Big brother.
No comments:
Post a Comment