Wednesday, August 28, 2013

Bondia Francois Botha “The White Buffalo” live in Tanzania

Najua wengi walikua hawaamini kama ni kweli huyu Super star anakuja bongo ila
sasa ndio time ya kuamini baada ya bondia huyu staa wa dunia raia wa Afrika Kusini Francois Botha “The White Buffalo” kukanyaga ardhi ya JK kwa mara ya kwanza August 27 2013.

Alifanya interview na Jahazi la Clouds FM kwa zaidi ya dakika 20 na kuthibitisha kwamba kaja kuhudhuria pambano la Francis Cheka na bingwa wa dunia uzito wa kati WBU Mmarekani Phil “The Drill” Williams Ijumaa August 30 2013 Diamond Jubilee kugombea ubingwa wa dunia uzito wa kati WBF.
Pamoja na hilo pia Botha kathibitisha kwamba mwanzoni mwa 2014 atapambana na Evander Holyfield kwenye pambano ambalo litachezwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam Tanzania.
Kwenye hilo pambano la mwakani waandaaji wamethibitisha kwamba mwimbaji staa R Kelly amekubali kuja kufanya show ambayo itakua ndio mara yake ya kwanza kuja Tanzania pia.

No comments:

Post a Comment

ShareThis