Wednesday, August 28, 2013

Diamond kuzindua Video yake aliyo shoot Afrika kusini august 29 Serena hotel bila kiingilio


DIAMOND PLATNUM 2
Ni mazoea ambayo watu wake wamekua nayo kwamba akiwa na tukio kama hili basi ni lazima
atalifanya kwenye mojawapo ya club za usiku Dar es salaam kama alivyokua akifanya mara nyingi lakini this time staa huyu anaelipwa ghali zaidi kwenye show zake ambae pia siku zake za kupumzika mara nyingi ni jumatatu au jumanne ameenda kwenye levo nyingine.
Diamond Platnumz kesho August 29 2013 anategemea kuitambulisha kwa fans wake video yake mpya kabisa ambayo picha zake zilisambaa kwenye mtandao ambapo ameishoot Afrika Kusini na hili tukio litafanyika kwenye hotel ya kifahari Dar es salaam… Serena.
Serena hotel
Diamond mwenyewe anasema hakutakuwa na kiingilio kwenye uzinduzi huo lakini wataofika ni wale waliopewa mwaliko maalum kuingia kwenye hii hoteli maarufu ambayo ilizoeleka pia kuwahudumia mastaa wakubwa wa muziki kama Fabolous, Koffi Olomide na wengine lakini this time Diamond Platnums amekodi ukumbi alafu hataki watu walipe kiingilio, yani anaalika tu.
DIAMOND PLATNUM 2
1240001_535696829842915_1667270827_n


No comments:

Post a Comment

ShareThis