Wednesday, August 21, 2013

Filamu ya Juma Nature na Sintah ‘Sitaki Demu’ kuingia sokoni hivi karibuni

Unakumbuka jinsi uhusiano wa Juma Nature na Sintah ulivyokuwa maarufu miaka ya 2000? Enzi hizo, huu ndio ulikuwa uhusiano uliokuwa ukiandikwa sana kwenye magazeti, kama ilivyokuwa Diamond na Wema Sepetu.
page

Kuachana kwao kulizalisha hits mbili za Nature, Sitaki Demu na Inaniuma Sana ambazo zote zilikuwa zikimhusu Sintah. Na sasa filamu itakayotowakutanisha tena wapenzi wa zamani, Sitaki Demu ipo njiani kuingia sokoni.

Akiongea na Clouds E ya Clouds TV, Nature amesema filamu hiyo itakayoonesha namna uhusiano wao ulivyokuwa enzi hizo, inatarajia kutoka mwezi October. Amesema filamu hiyo ni maalum kwaajili ya mashabiki wao.


No comments:

Post a Comment

ShareThis