Wednesday, August 14, 2013

Hatimaye Chidy Benz amsamehe Baghdad na video ya “Wambie Nipo” kutoka hivi karibuni

baghdad 

 Baada ya msanii Baghdad kufanya collabo na Chidy Benz pamoja na Nay Mitego bila wao kujua, Chidy alikataza video yake kutoka. Kama ulikuwa hujui ni kwamba wote wawili walifanya video hii katika location tofauti, hakuna hata mmoja aliyemuona mwenzake wala kujua isipokuwa Baghdad ambaye ndiye mwenye hiyo ngoma.



Vyanzo vyetu vya habari vinasema kwamba director na editor wa video hiyo alikatazwa kuitoa hiyo video kwasababu Chidy hakupendezwa na mchezo uliofanyika lakini audio yake ilitoka. 

Millardayo.com ikizungumza na Baghdad mwenyewe alisema kitu ambacho kimetokea baada ya juhudi za mama yake kusaidia,

”Mama alijaribu kuwasiliana na Chidy Benz lakini Chidy alikuwa na safari zake nchini Kenya. Baada ya kurudi aliendelea kumtafuta nadhani walikutana au kumaliza kila kitu kwenye simu. Chidy alimuelewa mama na akamwambia aniambie kitu kilichotokea hakukipenda. Wasanii wengine labda wangezuia hiyo video isitoke tena lakini yeye amenisamehe na kanipa ruhusa ya kuitoa. So, shukrani zangu zimfikie yeye na mama kwa kufanikisha video hii kutoka”.

Oky, so lini fans wako na wa muziki wa bongoflava wategemee kuiona hiyo video,“Jinsi ilivyopitia mambo mengi hii video inabidi tuizindue kwa style ya pekee. Nimeongea na Maisha Club kuhusu uzinduzi wa video hii. Wananipangia tarehe ya kuizindua kati ya tarehe 25/8 au tarehe 1/9 nitaizindua pale Maisha Club na kila mtu ataiona kuanzia hapo”.

Use Facebook to Comment

ShareThis