Kanye West na Drake wamekutana kwenye stage pamoja ndani ya ardhi ya Toronto Canada.
Uliwahi kusikia watu wakisema mastaa hawa wa hiphop..................
wana beef? Kama jibu lake ni ndio, basi naomba kukufahamisha baada ya kumnukuu Drake.
Anakwambia hakuna ugomvi kati yake na Kanye West, ni basi tu kila mmoja amekua busy kutafuta pesa… hata hivyo pia ukaribu wao sio kihiiiiivyo.
‘Siongei sana mara nyingi na Kanye west kama ninavyoongea na Lil Wyne au P Diddy, hatuwasiliani kwa sana kiiihivyo ila namuheshimu na naiga mengi kutoka kwake’ Drake.
Good news ni pale Kanye West alipokatisha muziki na kutoa maneno mazito kwenye stage ya kumsifia Drake, maneno yaliyomfanya Drake kudiriki kusema anaona kama ndoto vile, yani kama ndio anaamka asubuhi…. Kwa sababu Kanye West na Jay Z ni kama miungu kwake, sasa kusifiwa kama hivyo nikitu kikubwa sana.
Kanye West alikiri kwamba rapper mdogo mwenye umri wa miaka 26 tu Drake, alichangia kuwapa presha, yani anakimbiza kwenye game mpaka Kanye na Jay Z ambae ni role model wa mastaa wengi tu wa Tanzania, wakaamua kuungana na kujipanga na kufanya album ya watch the throne.
Yani ujazo wa Drake kwenye game ni mkubwa mpaka wakongwe wakimsikiliza wanasema hata kuingia inabidi tujipange mazeee..