Wednesday, August 14, 2013

Model Ally Daxx apata dili mpya kwenye modeling huko South Africa


35000_633377416676221_1915204312_n 

Mtanzania Ally Daxx ambaye anafanya kazi ya modeling nchini South Africa kwenye agency ya Ice Model management, ambapo alifanikiwa kufanya matangazo ya Aston Martin, Alfa Romeo na mengine mengi. Hivi karibuni alisema  kwamba mkataba wake na agency  ya Ice Model unakaribia kuisha na anajaribu kufanya mawasiliano na agency ambazo ziko Marekani.


Habari kutoka kwa Daxx anasema kwamba agency hiyohiyo ya Ice Model imeridhishwa sana na kazi yake kwa muda wa mwaka mmoja aliofanya na wamempa mkataba mpya wenye maslahi mazuri zaidi. Daxx ambaye ndiyo model pekee wa kiume anayeiwakilisha Tanzania kwenye anga za kimataifa anasema, “Nime-sign mkataba wa miaka mitatu wa kuendelea kufanya kazi na Ice Model management.Muda mfupi niliofanya nao kazi umenipa profile kubwa naamini miaka 3 ijayo nitakuwa pazuri zaidi”.

Use Facebook to Comment

ShareThis