mara nyingine hapa Bukoba Tangu azushiwe na wadau kwamba alifariki Dunia katika ajali ya boti miezi michache iliyopita.Saida kajitokeza kuthibitisha kuwa habari hiyo ilikuwa ya uzushi mtupu na ya uongo. Leo hii Jumamosi akiwa amesindikizwa na wasanii wa Nyumbani kwao Bukoba Bk Sande, Papaa Kishaju, pamoja na wanamuziki wa VISION MUSIC AMBASSADOR wanaodhaminiwa na 100.0 Vision fm Radio BUKOBA na Kundi la Ka Jay Poda kutoka Kenya amabo wameusindikiza usiku wa SAIDA KAROLI vilivyo na kukamua kisawasawa.
Saida na Wanamuziki wake wakiendelea kuimba
Bw. Willy O Rutta ( Kiroyera) kulia na Bw. Ernest Nyambo wakicheki kisawasawa burudani
Dada akibaki mdomo wazi huku akiwa aamini macho yake kwa kile alichoburudishwa kutoka kwa msanii mkongwe Saida Karoli.
Kesho Jumapili Tarehe 8.9.2013 Saida ataendelea kwenye tamasha la pili katika uwanja wa Kaitaba Kiingilio ni Tsh.2500/= tu. Saida Karoli atasindikizwa na Jopo la wasanii lukuki waliowahi kurekodia nyimbo zao ndani ya Tivol Studio wakiwemo wasanii wa nchi Jirani na wa hapa nyumbani Bukoba.
No comments:
Post a Comment