Saturday, November 30, 2013

Nay wa Mitego: Natamani kufanya ngoma na Rabbit, Octopizzo, Sanaipei, Avril na Mejja


Nay wa Mitego amewataja wasanii wa Kenya anaopenda kufanya nao ngoma wakati akiongea kwenye kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen na mtangazaji Willy M Tuva.
379faee459a711e39ae812f4c87253a8_7
Akiwataja wasanii hao, Nay alisema anatamani kufanya kazi na Sanaipei na Avril na kuongeza kuwa msanii anayempenda zaidi nchini Kenya ni
Mejja.
Kwa upande wa Hip Hop alisema angependa kumshirikisha Octopizzo na Rabbit.
“Hawa watu tukikaa hapa tukipata na mtoto wa kike katikati akatufanyia kitu chake itakuwa ni collabo ya Afrika Mashariki,” alisema.


No comments:

Post a Comment

ShareThis