Wednesday, December 18, 2013

Picha: Barnaba boy Avuta Mkoko mpya


Bado huamini kwamba muziki wa bongo sasa unalipa? Kama umejibu ndiyo nakushauri u-update fikra zako sababu wasanii wa miaka ya sasa wamekuwa wakionesha mafanikio ya aina mbalimbali yanayotokana na kazi ya muziki wanayoifanya.
mark x-3
Barnaba wa THT leo ameonesha ‘mkoko wake’ mpya kupitia
Instagram, tena akiwa bado hata hajapewa ‘birth certificate’. Ameionesha gari yake mpya aina ya Toyota Mark X ikiwa bado na chasis namba na kuandika “Oyeaaaaa Thanx Lod imetimia”.
mark x-2
Katika picha nyingine Barnaba a.k.a baba Steve aliandika “New”, na picha ya tatu aliandika “Kaz nzuri na mambo mazuri”.
mark x-1


No comments:

Post a Comment

ShareThis