Saturday, December 28, 2013

Picha: Wateja wa Vodacom walivyojirusha kila kona ya jiji la Dar kwenye Krismasi


001 COCO
Chege akionyesha umahiri wake wa kutawala jukwaa wakati wa Tamasha la
Cheka Bombastiki lililofanyika katika ufukwe wa Coco beach jijini Dar es Salaam mahususi kwaajili ya wateja wa Vodacom na uzinduzi wa simu za mkononi za Huawei kwaajili ya wateja wao wakati huu wa sikukuu ya Krismasi
002 COCO
Mpiga picha Mkuu wa Gazeti la Changamoto Albart Jackson akionesha simu aina ya Huawei Y210D yenye thamani ya Tsh. 160,000 kwa waandishi wa Habari aliyojishindia kwenye bahati nasibu iliyowahusisha waandishi wa habari,wakati wa Tamasha la Cheka Bombastiki lililoandaliwa mahususi kwaajili ya wateja wa Vodacom na uzinduzi wa simu za mkononi za Huawei wakati huu wa msimu wa sikukuu,Kulia ni Mtaalamu wa bidhaa na Vifaa vya simu wa Vodacom Edwin Byampanju na kushoto ni Meneja Masoko na usambazaji wa Huawei Ramadhani Hamad
003COCO
Mmoja wa wasichana waliokuwa wakipromoti simu za Huawei akipita jukwaani huku akionyesha moja ya simu za Huawei wakati wa Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa mahususi kwaajili ya wateja wa Vodacom na kuzinduliwa kwa simu za mkononi za Huawei wakati huu wa msimu wa sikukuu, katika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam
004 COCO
Msanii wa kundi la Tiptop Connection Madee akiwaburudisha mamia ya wakazi wa jiji la Dar es salaam waliofurika katika ufukwe wa Coco Beach
005 DAR LIVE
Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya Profesa Jay akiwapagawaisha mashabiki waliofurika katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam, wakati wa Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa na Vodacom Tanzania na Serengeti kwaajili ya wateja wao wakati huu wa msimu wa sikukuu ya krismasi
006 DAR LIVE
Kiongozi wa bendi ya muziki wa kundila la Jahazi Modern Taarab Mzee Yusuph akikonga nyoyo za mashabiki wake wakati wa Tamasha la Cheka Mbombastik lililofanyika katika ukumbi wa Dar Live mbagala jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Krismasi Tamasha hilo liliandaliwa na Vodacom Tanzania na Serengeti
007 COCO
Umati wa watu waliofurika katika ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam, wakati wa Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa na Vodacom Tanzania
008 DAR LIVE Joe
JoH Makini akionyesha umahiri wake kwa mashabiki wa muziki huo wakati wa Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa na Vodacom Tanzania na Serengeti Breweries katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam mahususi kwaajili ya wateja wao wakati wa msimu huu wa sikukuu ya krismasi



No comments:

Post a Comment

ShareThis