Wednesday, December 18, 2013

Wasanii wa Nigeria Banky W na Tiwa Savage waanzisha TV Talk show yao ‘The Banky & Tiwa Show’


Unapozungumzia wasanii wakubwa na wanaoheshimika katika kiwanda cha muziki cha Nigeria na Afrika, majina ya mwimbaji wa ‘Yes/No’ Banky W na staa mrembo aliyekuwa bibi harusi hivi karibuni, hit maker wa ‘Kele Kele’ Tiwa Savage hayawezi kukosekana. Mastaa hao wameunganisha umaarufu wao na vipaji vyao vya muziki na kuanzisha TV Talk show yao ‘The BANKY & TIWA SHOW’.
Tiwa n B
‘The BANKY & TIWA SHOW’ ni talk show itakayokuwa
ikihusisha topic zinazohusu mambo mbalimbali controversial katika jamii za Waafrika kama vile ulevi, ushoga, kuvunjika kwa ndoa, uzinzi, Pastors, Private Jets na mengine mengi.
Wageni wa kipindi hicho watakuwa wakibadilika kuanzia kwa wasanii wa muziki, waigizaji, watangazaji wa radio na TV (of course za Naija), na watu wengine maarufu.
banky n Tiwa
Tiwa Savage na Banky W
Producer wa kipindi hicho Adeola Oloyede amesema ‘The Banky & Tiwa Show’ kitakuwa cha kwanza cha aina yake, “For the first time, we are getting a glimpse into the minds of our celebrated stars in the entertainment industry, through The Banky & Tiwa Show. The programme is fun, informative and entertaining, it is peeling back”, alisema.
Kipindi hicho ambacho kimeanza kuonekana jana (Dec 17) kitakuwa kikirushwa kupitia CHANNEL 165 kwenye DSTV.
Tazama Trailer ya kipindi hicho

Source: 360 Nobs



No comments:

Post a Comment

ShareThis