Monday, April 7, 2014

Roma adai kuna media zinakataa kupiga wimbo wake ‘KKK’ mpaka afute baadhi ya maneno


Roma Mkatoliki amefunguka kwa kusema kuwa wimbo wake mpya ‘KKK’ unaendelea kufanya vizuri licha ya kuwepo kwa baadhi ya media ambazo zimekataa kuupiga mpaka afute baadhi ya vipande katika wimbo huo.
Roma kkk
Akizungumza leo Roma amesema kwa kuwa anahitaji wimbo wake upigwe kwenye media zote amelazimika kufuta baadhi ya vipande hivyo.
“Nashukuru mungu wimbo wangu umepokewa vizuri na unapigwa sehemu mbalimbali, katika media mbalimbali ingawa
kunachangamoto ambazo nimekutananazo. Kwa mfano kuna media ambazo zinaniambia hatutapiga wimbo wako mpaka ufute baadhi ya sehemu, kwa hiyo ili kwenda nao sawa unafuta halafu unawapelekea.” Amesema Roma.
Upande mwingine Roma amewashukuru madereva bodaboda na bajaj waliomsaidia kuufikisha wimbo wake mbali.
“Lakini kikubwa zaidi nawashukuru sana madereva bodaboda na bajaj kwa kuwezesha muziki wangu kufika mbali zaidi,unajua watu walikuwa wanasubiria Roma baada ya ukimya atakuja vipi? Ila namshukuru Mungu mambo yameenda poa” Alisema Roma
Pia Roma amedai kuwa hii ni mara yake ya kwanza kupata interviews nyingi sana baada ya kutoa wimbo wa KKK kuliko nyimbo zake zote.

No comments:

Post a Comment

ShareThis