Matumaini ya Tanzania (na Afrika Mashariki) kuibuka mshindi katika shindano la Big Brother Africa (Big Brother The Chase) linaloendelea yamepungua na kubakia mikononi mwa mshiriki mmoja tu aliyebakia ndani ya Jumba la Big Brother.
Nando out of The Chase
Matumaini hayo yamefifia baada ya mshiriki kutoka Tanzania, Nando, kuenguliwa katika shindano hilo kutokana na vitisho vya kauli na vitendo alivyovionyesha ndani ya jumba hilo kwa mshiriki mwingine,Elikem kutoka Ghana. Mojawapo ya makosa ambayo yamemuondoa Nando ndani ya jumba ni pamoja na kutoa vitisho vya kauli kwa mshiriki huyo kutoka Ghana akidai “watu kama Elikem hawastahili kuishi” na kisha kukutwa amelala na mkasi chini ya mto kitu ambacho kinaashiria alikuwa amedhamiria kudhuru.Vitendo vya fujo na vitisho ni miongoni mwa mambo ambayo Big Brother hana masihara nayo kabisa.
Nando anakuwa mtanzania wa pili kutolewa katika shindano hilo kutokana na “tabia mbaya” kwani kama mtakumbuka wakati wa shindano la mwaka 2011 la Big Brother Amplified, mshiriki Lotus alitolewa baada ya kumnasa mshiriki mwingine makofi.
Kuenguliwa kwa Nando kunamaanisha kwamba mshiriki Feza (mwingine anayeiwakilisha Tanzania mwaka huu) ndiye pekee aliyebakia ndani ya Jumba la Big Brother akiipeperusha sio tu bendera ya Tanzania bali pia Afrika Mashariki nzima baada ya washiriki wengine wote kutoka Kenya na Uganda kutolewa mapema tu.
Wakati wa Live Eviction show mapema hivi leo,washiriki Annabel kutoka Kenya na Sulu kutoka Zambia waliaga shindano. Unaweza kucheki zaidi kuhusu yanayojiri ndani ya Big Brother-The Chase kwa kubonyeza hapa.
No comments:
Post a Comment