Monday, July 22, 2013

Makala: Ingekuwa Vipi? (Mwana FA): Miaka 12 Baadaye

 Wakati anarekodi Ingekuwa Vipi? Mwaka 2001, Hamis Mwinjuma aka MwanaFA alikuwa kijana mdogo mwenye miaka 21 tu. Kama zilivyo ndoto za wasanii wengi wachanga, yeye pia alikuwa na hamu kubwa ya kutaka kutoka lakini mambo hayakuwa rahisi.
mwanafalsafa
Kilikuwa ni kipindi ambacho amemaliza tu high school na akijipanga kwenda kusoma chuo. “Nilikuwa nyumbani tu, nilikuwa idle idle mno,” Mwana FA anakumbushia.
Mwaka 2000 alikutana na producer aliyemtoa Bonny Luv, mitaa ya Upanga jijini Dar es Salaam na alikuwa anamfahamu kitambo na kumchukulia kama kaka yake. Alikuwa akifahamu kuwa ni producer hivyo mara kwa mara hakuchoka kumfuata kumshawishi amsaidie.
“Kanisikiliza sana jamaa, akawa anasema ‘bwana mi nataka kurudi kule’ kwasababu wakati huo alikuwa amefunga studio yake, lakini akawa anasema ‘mimi nataka kurudi kuanza kufanya upya’ anasema FA.


Bonny Luv alimwambia FA kuwa amepanga kwenda nchini Uingereza kuchukua masomo ya Sound Engineering.

Mwishoni mwa mwaka 2001, Bonny alikamilisha safari yake na kwenda nchini Uingereza ambako alikaa kwa mwaka mmoja huku nyuma FA akibaki kumsubiria.

Akiwa nchini humo, Bonny alichukua kozi hiyo lakini pia aliamua kununua vifaa vipya vya studio yake vya kuanzia alivyokuja navyo mwaka 2001 na ndipo ndoto ya kurekodi ya Mwana FA ilianza kuonesha dalili njema.
“Tulikuwa tumeshakubaliana kimsingi kwamba mimi ntakuwa msanii wake, ntafanya kazi chini yake kwahiyo ‘be patient’ kwahiyo mimi nikawa namsubiria yeye.”
Hata hivyo kumsubiri Bonny kwa mwaka mmoja wakati akiwa masomoni nchini Uingereza, hakukuwa rahisi kwa FA hasa kwakuwa alikuwa na hamu kubwa ya kurekodi wimbo.
“Unajua mtu kama Profesa Jay, mimi najuana naye siku. Kuna kipindi nilikaa kwa babu yangu Kimara kwahiyo alikuwa jirani yangu, toka Profesa naye mwembaba kaka mimi (kicheko). Sasa Profesa akawa anajua mimi naweza. Wakati huo Profesa anafanya kazi Mobitel Tanga. Akaniambia alikuwa anarekodi albam yake ile, Machozi, Jasho na Damu.
Akaniambia ‘bana nenda kwa Majani pale kuna wimbo unaitwa Na Bado ukaingize verse pale’. Sasa ilikuwa nifanye mimi, Profesa na jamaa wengine wawili sijui walikuwa nani na nani. Kwahiyo mimi nikawa na verse yangu kabisa, nikaenda mpaka kwa Majani, Majani akanizungusha sana, mara sijui umeme umekatika, lakini I understand now kwasababu ananiona mimi underground, anaona hizi zitakuwa fujo zile zile. Kama mimi hapa ninavyosumbuka kwamba ‘mimi nina nyimbo yangu sijui nataka unitoe nini, I understand position aliyokuwa nayo wakati huo. 

Kila siku naenda, njoo kesho, mpaka miezi mitatu hivi jamaa ananigalagaza. Mwisho siku moja nikamkuta pale.. unajua pale ukiwa unaenda kwa Majani kuna bar hapa kwenye kona. Nikamkuta Majani pale akaniambia ‘bana huu wimbo watu wengine wawili wameshaingiza na Profesa wa tatu kwahiyo we can’t have that wimbo uwe mrefu hivyo, kwahiyo wewe naona kama nafasi yako haipo hapa’, akanimwaga yaani.
Lengo langu mimi, nafikiri hata Profesa lilikuwa hilo, yaani nikafanye verse hii kwa Majani, Majani angeniona lazima angening’ang’ania. Unajua ile verse yangu ya Na Bado nilikuja kuweika kwenye nini? Ile verse yangu ya ‘Hii Leo. Kama angejitolea kunisikiliza, pengine ningekuwa msanii wa Majani, yaani ningetokea kwa Majani kwasababu hiyo Bonny alikuwa amekaa mwaka mzima na unajua uvumilivu wa wasanii wachanga na watu wanaotaka kutoka unakuwaga mdogo. So Majani alipokataa mimi ikabidi niendelee kusubiri tu.”
Baada ya Mwana FA kuhamisha makazi yake kutoka Upanga na kwenda kuishi Kijitonyama, alimkuta Jay Mo akiishi huko na wakawa majirani. Wakati huo Jay Mo alikuwa na wimbo mmoja tu redioni. Mwana FA na Jay Mo wakawa washkaji. 

Jay Mo aliisikia idea ya Ingekuwa Vipi na akaipenda na kumtaka FA aweke verse zake. FA anasema hilo lilikuwa wazo zuri kwakuwa kipindi hicho mitindo ya kubadilishana bars kwa bars (shifting) ilikuwa imeshika kasi.
“Jay Mo alikuwa ameshasikika na ni aina ya muziki ambao nilikuwa nausikiliza. Kuna kipindi hizi hardcore rap hizi kabisa zilikuwa na deal kwelikweli.

Kwahiyo kufanya wimbo wa Jay Mo mimi ilikuwa opportunity lakini pia kufanya wimbo tunafanya shifting ilikuwa kitu kizuri na kuongeza mtu, kama nilikuwa sijiamini hivi kama naweza kutoka mwenyewe, nikaona labda niongeze mtu kuongeza impact ya hii kitu.”
Ilipotoka Ingekuwa Vipi, jina la Mwanafalsafa lilivuma kwa kasi nchini na kwa kipindi kifupi jina lake likawa likizungumzwa kila kona nchini.

“Unajua baada ya Ningekuwa Vipi, kila kitu kilienda nuclear. Nakumbuka nilisoma gazeti moja hiyo 2002 jamaa walisema ‘kutoka weekend mpaka wakati tunaenda kulichapisha hili gazeti, (ni magazeti yale ya Ijumaa), Jumatano, wimbo wa Ingekuwa Vipi wa Mwanafalsafa na Jay Mo umepigwa kwenye radio tofauti mara 72’, yaani nakumbuka haijawahi kunitoka kichwani mpaka leo, kwasababu nywele zilinisisimka hivi.
(Ingekuwa Vipi) ni ule wimbo ambao mmoja umetoka, ukawa mkubwa moja kwa moja na shughuli ikaishia hapo kukawa hakuna struggle za watu kutaka kutoka tena, ni watu kuprove tu kwamba wanaweza tu.
Huo ndio ulikuwa mwanzo wa muziki wangu yaani kila kitu kilianzia hapo.”



No comments:

Post a Comment

ShareThis