Saturday, August 24, 2013

Hatimaye ‘North West’ awekwa hadharani kwa mara ya kwanza (picha)

Ikiwa ni takriban miezi miwili ipite toka rapper Kanye West na Kim Kardashian kuwa wazazi baada ya kupata mtoto wa kike aitwaye ‘North West’, jana ndiyo siku ambayo picha ya mtoto huyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu iliwekwa hadharani kwa mara ya kwanza.


North west North West

Baada ya kukataa offer za pesa nyingi kutoka makampuni mbalimbali yaliyotaka kuzipata picha za mtoto huyo mapema toka alipozaliwa (June 15), baba mtoto Kanye aliweka hadharani picha ya mwanae kupitia kipindi kipya cha mama mkwe wake kinachoitwa ‘Kris Jenner’ kilichoruka jana (August 23).

Baada ya kipindi kuruka mama yake Kim aitwaye Kris alitweet picha hiyo ya mjukuu wake na kuandika “Meet North West”.

Kanye ndiye alikuwa mgeni katika talk show mpya ya ‘Kris Jenner’, na kipindi cha jana kilikuwa na umuhimu mkubwa kwa Kris kwasababu ndio kilikuwa cha mwisho kabla kituo cha TV FOX kutoa maamuzi ya kuendelea nacho ama laa.

Hivyo uwepo wa Kanye pamoja na kumuonesha North West katika show hiyo huenda vikawa na thamani kubwa zaidi ya zile offer ambazo Kanye na mpenzi wake Kim walizikataa kwaajili ya kutoa picha ya mwanao. Familia imezingatiwa kwanza.

Tupe maoni yako baada ya kumuona mtoto wa Kanye West na Kim Kardashian.


No comments:

Post a Comment

ShareThis