Saturday, August 24, 2013

NDEGE ILIYOLAZIMIKA KUTUA ZIWA LA MANYARA BAADA YA INJINI MOJA KUFELI


 DJ SEKNdege ya shirika la ndege la Tanzanianair ikiwa imetua katika maji ziwa Manyara jana na abiria saba kukimbizwa hospitali mkoani Arusha baada ya injini moja kushindwa kufanya kazi ikiwa angani.


Ndege Ndogo ya Shirika binafsi la Ndege la TANZANAIR iliyokuwa ikitokea Mjini Bukoba kuelekea Jijini Dar es Salaam kupitia Zanzibar, imelazimika kutua katikati ya Ziwa Manyara lililopo Mkoani Arusha ili kunusuru abiria wake sita (6) waliokuwamo katika ndege hiyo baada ya kupatwa na hitilafu kwa kuzima ghafla kwa Injini moja wakati ikiwa hewani. 
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Kamanda Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa ajali hilo majira ya saa 2.35 asubuhi maeneo ya Lambi, kusini mwa wilaya ya Babati. 
 Kamanda Sabas  amesema rubani wa ndege aliyetajwa kwa jina moja la Kondo, ambaye hakudhurika katika ajali hiyo, alitaka kutua ghafla katika viwanja vya  Arusha na Manyara baada ya kutokea hitilafu hiyo, lakini alishindwa baada ya kuona mtikisiko ukizidi na kuamua kuielekeza ndege hiyo katikati ya Ziwa hilo, ambapo alifanikiwa kutua salama.
Baadhi ya Boti na mitumbwi iliyokuwa karibu ilisogea na kutoa msaada wa kubeba abiria hao na kuwasogeza nchi kavu na baadaye ilifika Helikopta ambayo iliweza kutoa msaada zaidi.


DJ SEK BLOG


No comments:

Post a Comment

ShareThis