Friday, August 23, 2013

SEMINA YA FURSA KWA VIJANA ILIVYOPOKELEWA LEO MKOANI KIGOMA



Mghani mahiri wa mashairi hapa nchini Mrisho Mpoto akizungumza kwa msisitizo,masuala ya fursa mbalimbali zinazopatikana katika suala zima la ujasiliamali mapema leo kwenye semina ya Fursa iliyofanyika katika ukumbi wa  Student's Center,uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora mapema leo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 
  Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,akizungumza mbele ya washriki wa Semina ya Fursa ndani ya ukumbi  kwenye ukumbi Student's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora.
 Baadhi ya Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakishiriki semina ya Fursa kwa vijana ililiyofanyika leo kwenye ukumbi wa Student's Center katikati ya mji wa mkoa wa Tabora mapema leo,kutoka kulia ni Msanii Godzilla,Baba Levo,Amin,Stamina na wengineo.

 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Mwasiti Almas akizungumzia baadhi ya fursa alizozipata mara baada ya kujiunga na shirika la NSSF,mbele ya Washiriki wa Semina ya Fursa (hawapo pichani),kulia kwake ni Mwakilishi wa NSSF-Makao Makuu Bwa,Salim Khalfan akimsikiliza kwa makini.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil.
 Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya mafuta-Lake Oil,Bwa.Ben Temu akizungumza kwenye semina ya Fursa,ambapo yeye alielezea mambo mbalimbali ikiwemo suala la vijana kuwa wenye moyo wa kujituma na kutokata tamaa mapema,alieleza kwa kuwataka vijana wawe wavumilivu na kuachana na tabia ya kujiona hawawezi kufanya jambo,kwamba kila fursa wanayokumbana nayo waitumie vizuri katika suala zima la kujikwamua na kujiendeleza kimaisha. Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 
 Sehemu ya Meza kuu.Kutoka kushoto ni Wawakilishi kutoka shirika la NSSF,Salim Khalfan (makao makuu),Alloys Banigwa (Meneja wa NSSF-Tabora),Mkuu wa Wilaya ya Iramba kutoka Mkoani Singida,Mkuu wa Wilaya ya Igunga,Mh.Elibarik Kingu,Ruge Mutahaba-Clouds Media Group, pamoja na Ben Temu kutoka kampuni ya Lake Oil.


 Semina ya Fursa ikiendelea mapema leo ndani ya ukumbi wa Student's Center katikati ya mkoa wa Tabora mapema leo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil.
 Mwakilishi wa Shiriki la NSSF kutoka Makao Makuu jijini Dar,Bwa.Salim Khalfan akielezea fursa mbalimbali zinazopatika mara mtu yeyote anayejiunga ama amejiunga na NSSF,alifafanua zaidi kuwa mtu yeyote atakayejiunga na shirika hilo atanufaika na mambo mengi,ikiwemo suala la matibabu,mikopo na mengineyo lukuki yanayopatikana ndani ya shirika hilo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 

No comments:

Post a Comment

ShareThis