Monday, August 26, 2013

tamasha la serengeti fiesta 2013 Ilivyokuwa usiku wa jana ndani ya singida motel mkoani Singida.



Msanii wa muziki wa kizazi kipya ajulikanae kwa jina la kisanii kama Rachael akitumbuiza jukwaani usiku huu mbele ya umati mkubwa (hawapo pichani) wa wakazi wa Singida na vitongoji vyake ndani ya Singida Motel,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea.

 Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Singida wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 linalofanyika kwenye viwanja vya Singida Motel usiku huu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Petter Msechu akiwaimbisha mashabiki wake waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013 linaloendelea hivi sasa ndani ya Singida Motel.
 Ni ndani ya Singida Motel tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea hivi sasa .
 Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Lina na Amin wakilishambulia jukwaa kwa pamoja,huku wakazi wa Singida waaliofurika usiku huu ndani ya Singida Motel wakipiga mayowe ya shangwe.
 Amin Jukwaani akiwambisha mashabiki wake,huku mayowe kila kona yakisikika usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya Singida Motel,mkoani Singida.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Abdul Kiba akiimba jukwaani kwa hisia usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013,ndani ya Singida Motel usiku huu mkoani Singida. 
Ni burudani Serengeti Fiesta nomaa sanaaa usiku huu,

No comments:

Post a Comment

ShareThis