Saturday, September 14, 2013

Video na taarifa za Padre Ancelmo Mwang’amba kumwagiwa tindikali Zanzibar


1371450_10200746553170104_445747008_n (1)

Taarifa kutoka Zanzibar zinasema Padre Ancelmo Mwang’amba wa kanisa Katoliki Zanzibar amemwagiwa tindikali na watu wasiofahamika akiwa anatoka kwenye huduma ya internet aliingia tena ndani ya cafe huku akiwa amejishika uso na muda mfupi baadae mtu akaingia na kusema mzee huyu amemwagiwa tindikali.
Baadhi ya watu walimkimbiza padre huyu kwenye hospitali kuu ya Zanzibar Mnazi mmoja ambapo Madaktari wanasema tindikali hiyo amemwagiwa sehemu za usoni na kwenye kifua.
Padre Ancelmo anafanya kazi kwenye kituo cha kulelea vijana ambacho kipo chini ya kanisa Katoliki ambapo hili linakuwa ni tukio la tano la watu kumwagiwa tindikali Zanzibar baada ya Mkurugenzi wa manispaa Rashid Ally,Katibu wa Mufti, Raia wa wawili wa uingereza na hadi hivi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kwa kuhusika na haya matukio.

No comments:

Post a Comment

ShareThis