Wednesday, October 2, 2013

Audio: Jinsi Chidi Benz na Cassim walivyowashiana Moto Club Billicanas

Hivi karibuni Chidi benz  na ney wa mitego walipatanishwa  kwakumaanisha hapatakuwa na tofauti kati ya wawili hao.ila  Kilichotokea sasa ni kwamba, Chidi Benz anamuita Cassim Mganga Mchawi, kauli ambayo ambayo iliwafanya hivi karibuni watukanane matusi ya nguoni Club Billicanas, na kama wasingekuwepo watu waliowazuia, wangetoana meno siku hiyo.
IMG_9071

“Mwacheni asinizingue mimi, nakosea mimi kila siku,” anasikikia Cassim akiongea kwenye audio iliyorekodiwa na kuifikia mikono ya Soudy Brown wa U Heard. “Mimi nimekosea nini Benz apige was**ge wengine mimi hawezi kunifanya lolote, msimshike, aniguse halafu aone. Mimi si maisha yangu, nahangaika nafanya muziki wangu wanasema mimi mchawi, mimi nina familia yangu, mimi sio mchawi, namroga nini mimi, yeye stress zake, anavuta unga, mimi namsingizia? Kila mtu anajua, yeye si life yake amechagua? Asinizingue, mimi mwanaume power kama yeye.”
Sikiliza mwenyewe hapa.

No comments:

Post a Comment

ShareThis