Wednesday, October 9, 2013

Crunk Views: Mambo Kumi yakuzingatia kabla hujafika Miaka 26.

Soma hapo chini  Mambo 10 ya kufanya kabla hujatimiza miaka 26.

 
kutokana na mambo mengi vijana kutoya fahamu na kuwasababishia mambo yao mengi kwenda ndivyo sivyo katika maisha na kujikuta wanaingia kwenye njia ambazo za tofauti ili kufanikisha kile wanacho hitaji,hivyo Bongo Crunk entertainment imeanda kitu kipya kwa vijana (Crunk Views) ili iwaweke kwenye njia iliyokuwa sahihi.

 Sasa hii ni kwajili yako  Ikiwa wewe ni kijana ambae hujafika au una karibia miaka 26  ni vyema ukafuata mambo kadhaa tuliyo orodhesha hapo chini:

Mambo 10 ya kufanya kabla hujatimiza miaka 26. 
1. Jifunze kuweka akiba ya fedha na iache bila kuigusa gusa.

 2. Tafuta mpenzi sahihi na tulia naye, panga maisha.

 3. Ishi mahali pa peke yako, acha kuishi kwenye nyumba au kupanga na washkaji. 

 4. Lipa madeni yako ya zamani. Yote! 

5. Tengeneza mwili ambao unataka halafu jitahidi ku-umantain! Anza kuzingatia kuishi kwa kujali afya yako sana.

 6. Jitahidi uwe na marafiki ambao wana changamoto za kimaendeleo zitakazokusaidia.

 7. Anza kujinunulia assets kama ardhi na nyinginezo. 

 8. Jifunze kuvaa vizuri na kwa heshima, si tu ilimradi umependeza.

 9. Kubali sasa kwamba umekua na acha tabia na mambo ya kitoto 

10. Yaache ya zamani yapite na anza mapya.

No comments:

Post a Comment

ShareThis