Friday, October 4, 2013

Exclusive Video: Young Killer adai kumjengea mama yake nyumba, mpaka sasa ameshatumia Mil 18

Hitmaker wa ‘Mrs Superstar’, Young Killer amesema ameanza kumjengea mama yake nyumba kama shukrani kwake kwa kumruhusu kufanya muziki.



Akizungumza na Bongo5 jana akiwa Tanga tayari kwa show ya Serengeti Fiesta mkoani humo, Killer alisema mama yake alikuwa akimkataza kufanya muziki lakini alikomaa tu na hivyo kumjengea nyumba ni ishara kuwa muziki sio uhuni bali ni ajira
Amesema nyumba hiyo ambayo hadi kukamilika inaweza kumgharimu takriban shilingi milioni 40, imemtoa mfukoni shilingi milioni 18 hadi sasa ilipofikia katika hatua ya Lenter.

“Lakini haijakamilika ipo nusu yake kwahiyo nimeshatumia kama milioni 18 hivi kitu kama hicho, kwahiyo naamini ntafanikiwa kuumaliza sababu ni special kwa mama yangu nataka aone matunda yangu ya muziki. Mara ya kwanza alikuwa hahitaji nifanye muziki lakini ameona nimenyanyua kidogo, kidogo anaelewa,” alisema Young Killer.

“Mafanikio sio gari tu, tunaanza na kujenga home na mambo mengine yanafuatia.”
“Haba na Haba hujaza kibaba, nilianza chini, nilitoka msingi, nimeenda hivyo hivyo, nikiwa napata lakini tano, laki mbili, laki ngapi, milioni kwahiyo najenga, naamini naimaliza.”

No comments:

Post a Comment

ShareThis