Friday, October 4, 2013

Mr Blue:Anaumizwa na mashabiki Wanaosema amepotea kwenye game ya Muziki

Harry Sameer aka Mr Blue amesema hakuna kitu kinachomuumiza kichwa katika muziki kama kuambiwa kapotea kwenye game.
293057_321562884564667_817489957_n
Alizungumza na Media ya  Bongo5 leo akiwa njiani akielekea
Tanga kutumbuiza kwenye Serengeti Fiesta, Mr Blue alisema amekuwa akikutana na maswali mengi na magumu kutoka kwa mashabiki kuhusu kupotea kwake kwenye muziki, kitu ambacho kimekuwa kikimuumiza kichwa.
“Muziki wa Tanzania umebadilika sana, wasanii ni wengi na kila mmoja anahitaji kuwa juu, kwahiyo mtu unatakiwa uangalie watu wako wanataka muziki wa aina gani ndiyo ufanye, ila ukifanyafanya tu utakuta unafanya ngoma nyingi halafu hazihit,” alisema rapper huyo.


No comments:

Post a Comment

ShareThis