Friday, October 4, 2013

Inspekta Haroun asema ana ndoto za kufungua gereji ya magari

Inspekta Haroun aka Babu amesema ingawa bado anafanya muziki, ndoto yake ya kuja kufungua gereji ya magari haijafa.
IMG_1403
Akizungumza na Media mbali mbali, rapper huyo wa
Mtoto wa Geti Kali, alisema anahitajikutimiza ndoto ya kufungua gereji kubwa ya magari ambapo kwa sasa imekuwa ngumu kutokana na pesa nyingi inayohitajika ili kukamilisha mpango huo.
“Mimi ni fundi magari wa muda mrefu na ndio fani yangu. Kwa muda mrefu nimekuwa na malengo ya kufungua gereji ya magari ila kikwazo ni pesa pamoja na shuguli zangu za muziki ila Mungu akinijalia nitafungua kwakuwa ni ndoto yangu ya muda mrefu,” alisema.
Katika hatua nyingine wiki hii Inspekta anatarajia kufanya uzinduzi wa wimbo wake mpya, ‘Sharubu za Babu’ utakaofanyika kwenye ukumbi wa Club Kakala Kigamboni jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

ShareThis